FAHAMU MAMBO YANAYO ENDELEA KUHUSU VITA UKRAINE NA RUSSIA
Moja ya washirika ambao walikuwepo jana katika Mkutano wa G7 uliofanyika Mjini Brussels nchini Belgium ni Katibu Mkuu wa NATO, Bw. Jens Stoltenberg.
Mambo yafuatayo yamepitishwa kwa lengo la kuisaidia Ukraine;
1. Kupeleka Misaada ya vifaa vya ulinzi wa kijeshi [cybersecurity assistance] ili kuisaidia nchi ya Ukraine kujilinda na Makombora ya Kibiolojia, Kemikali, Mionzi na Nyuklia.
2. Wamekubaliana kupeleka Majeshi katika nchi zilizopo Mashariki mwa Umoja wao wa NATO ili kuimarisha. i.e nchi ambazo zimetajwa ni Bulgaria, Hungary, Romania, na Slovakia.
3. Wameendelea kusisitiza na kuishauri China wasitoe msaada wowote kwenda kwa nchi ya Russia badala yake wameiomba China itumie ushawishi pamoja na urafiki wake na Russia kuimaliza vita hii.
4. Wamezishauri Taasisi pamoja Mashirika mbalimbali ya Kimataifa kutoshirikiana na Russia katika Masuala yote ya Kimaendeleo, Biashara na Uchumi kwa ujumla.
5. Wameshauriana kupunguza utegemezi wa kununua Gesi Asilia kutoka Russia, hapa Mbadala pekee ni kuanza kununua Liquified Natural Gas [LNG] kutoka Marekani i.e Matarajio ni leo wakamilishe dili hilo dhidi ya Marekani.
6. Wao kwa Pamoja wamesisitiza kwamba hawana chuki na wananchi wa Russia lakini kikwazo chao kikubwa ni Rais Putin ambaye amekuwa rafiki mkubwa na Rais wa Belarus, Lukashenko.
7. Wamezipongeza nchi jirani na Ukraine kwa kuendelea kuwapokea wakimbizi. Wameahidi kuzipa misaada ya Kifedha, madawa na vyakula katika kipindi hiki cha vita. i.e nchi hizo ni Poland, Slovakia, Hungary, Romania na Moldova.
8. Wameiomba Russia ifuate sheria za haki za binadamau pamoja na kufuata agizo la mahakama ya kimataifa la kusitisha Vita nchini Ukraine. i.e hii ni pamoja na kuondoa majeshi pamoja na silaha za kivita.
9. Wameionya Serikali ya Belarus kwa ushirika wao wa moja kwa moja katika vita hii wa kuisaidia Russia vifaa vya kijeshi na kupeleka majeshi nchini Ukraine. i.e ikumbukwe Russia na Belarus ni nchi rafiki sana.
10. Wameiomba nchi ya Russia kutotumia silaha za Nyuklia, Kemikali, Mionzi, na Biolojia kwasababu matumiizi yake yataharibu mazingira pamoja na kuchafua hali ya hewa ya dunia.
Post a Comment