KAMISHINA MSAIDIZI ARDHI KANDA YA DAR AIBUA FURAHA ZOEZI LA URASIMISHAJI WA ARDHI TEMEKE
Akizungumza kuhusu zoezi la urasimishaji wa ardhi, Kamishina Msaidizi wa ardhi kanda ya Dar es Salaam Bw. Idrisa Kayera amesema kuwa jumla ya wananchi 87,842 wametambuliwa.
Bw. Kayera aliendesha zoezi hilo la urasimishaji mbele ya wakazi hao kwenye mkutano wa wazi uliofanyika Kata ya Mbagala Manispaa ya Temeke.
"Leo tupo hapa katika kuendeleza zoezi la urasimishaji, sasa limekishwa tofauti na miaka ya nyuma kwani lilikuwa kero kwa wananchi" amesema Bw. Kayera.
Amefafanua kuwa kuna jumla ya makampuni 24 yanayofaya urasimishaji katika kata 14 za manispaa ya Temeke ambapo ina mitaa 46 ambayo tayari imefikiwa.
Amesema katika utekelezaji wa zoezi hilo, jumla ya viwanja 8,685 vimepimwa na kuidhinishwa na Wizara ya Ardhi, huku viwanja 24,714 vimewekewa (Beacon) na kazi bna viwanja 12,865 vimewasilishwa wizarani.
Kayera amesisitiza jamiii kuiga mfano wa watu wanaoambatana na wake zao na kuweka majina yao kwemye hati zao kwani hali hiyo ina ondoa migogoro wakati mmoja anapokuwa amefariki Dunia.
Hata hivyo amesisitza kuwa lengo kuu la umilikishaji hati miliki za ardhi litafanya Kila kitu kuwa na uhakika wa usalama wa umiliki wa ardhi na hivyo kuwainua wananchi kiuchumi Kwa kuwa hati miliki inamsaidia mwananchi kuaminiwa na taasisi za fedha na kukopesheka.
Afisa Mipango Wilaya ya Temeke Veronica Igoko aliyemwakilisha Mkurugenzi wa halmashauri hiyo, amesema amewaomba wajumbe wanyumba 50 watoe ushirikiano wa kutosha katika zoezi la Anuani za Makazi .
Amsesema urasimishaji wa makazi unaendelea na ifikapo Agusti 2022 kutakuwa na zoezi la sensa ya watu na makazi na kuwataka wananchi kujitokeza kwa wingi kuhesabiwa.
"Nawasihi sana wananchi waendelee kuchangia gharama za upimaji ili muweza kupata hati miliki , hii itarahisisha wakandarasi kufanya wajibu wao kwa urahisi na kuwawezesha wataalam wetu kurahisisha zoezi la ufuatiliaji na uwajibikaji na hatimaye hati ziendelee kutolewa."
Mwenyekiti wa Kibonde Maji kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) amesema zoezi hilo limefanyika kwa weledi mkubwa na kuwa limesaidia s wananchi.
Mkazi wa Yombo Vituka Bi. Pelepetua John Kibaja ni miongoni mwa wakazi waliopewa hati, amesema kuwa zoezi la kupata hatimiliki yake lilikua rahisi kwani alifuatilia ndani ya mwezi mmoja na kufanikiwa.
"Napenda kumshukuru Mungu kwa kupata hati hii nilitegemea ningekutana na changamoto nyingi, lakini haikua hivyo nimefanikiwa kupata kwa muda mfupi," amesema Bi. Pelepetua.
Mkazi wa Maji Matitu Kata ya Muanzini Herieth Rugemalira amefurahia kupata hatimiliki yake ya ardhi . "Nafuraha kwani niwanaume wachache wanaoweka majina ya wakezao katika utambuzi huu wa hati, ila mimi na mmewangu tulifuatilia pamoja na tumepata hati yetu inayotuonesha tunamiliki kiwanja chetu wote," amesema Herieth
Katika zoezi hilo kata za Chamanzi ,Toangoma,Makangarawe pamoja na Mbagala Kuu, Mianzini, harambe, Buza, Kijichi pamoja na kata zingine za Yombo Vituka na Kibondeni.
Post a Comment