Ads

FEDHA YA URUSI ( RUSSIA RUBLES) YAZIDI KUIMARIKA BAADA YA PUTIN KUTANGAZA KUIKATAA DOLA KATIKA MANUNUZI YA GES



 Tangu Machi 2, Rais wa Russia Vladmir Putin alipotangaza nchi yake ianze kuuza Gesi Asilia kwa kutumia fedha yao ya Kirusi [RUBLES], pesa yao imeongezeka thamani sana kwenye soko kuu la kubadilishia pesa la Moscow [Moscow Stock Exchange].


Putin aliongea jana na kusisitiza kwamba serikali yake ilichukua maamuzi hayo kwa ajili ya kukuza uchumi wa nchi yao, na tayari mambo yameanza kujipa kwani kwenye soko la kubadilisha fedha la Moscow pesa ya Russia [Rubles] imepanda thamani kuliko Dollar na Euro.

Fahamu hivi

Hadi kufikia Januari 27 Mwaka huu, Asilimia 58% ya mauzo ya kampuni namba moja ya uuzaji wa Gesi Russia, GAZPROM yalikua yanafanyika kwa Pesa ya EURO kwa mauzo yote ya Nchi za Ulaya pamoja na nchi chache duniani.

Ripoti za Mwaka Jana, hadi kufikia mwezi wa Tisa yaani Robo tatu ya Mwaka, Asilimia 39% ya Mauzo yao ya Gesi kwenda kwa wanunuzi mbalimbali duniani yalikuwa yanafanyika kwa kutumia pesa ya DOLLAR.

Hili linafanyaje kazi? Nchi itakayohitaji kununua Gesi Asilia kutoka Russia, itawalazimu kubadili fedha zao kwa kununua fedha za Kirusi [Rubles] kisha ndo waweze kufanya manunuzi ya Gesi Asilia. i.e kwahiyo uhitaji wa Fedha za Kirusi utaongeza thamani ya pesa hiyo.

Putin aliongeza kwa kusema, hili litawahusu pia mataifa yote ambayo siyo rafiki na Russia. Mwanzoni mwa mwezi Machi Putin alitoa orodha ya nchi 48 ambazo siyo rafiki na Russia. Nchi hizo ni wanachama wote wa Umoja wa Ulaya [EU] Marekani, Japan, Switzerland na Norway.

Mpaka sasa Germany na mataifa mengine ya ulaya yananunua Gesi Asilia kutoka Russia, hivyo tangu Machi 2 wamekuwa wakinunua Gesi kwa kutumia pesa ya Russia ndo maana ripoti za kichumi zinasema kwamba pesa ya Russia imeongezeka thamani.

Kwa mwaka 2021 pekee, Russia wamefanya Mauzo ya Gesi Asilia yenye thamani ya Takribani US $ 55.5 Billion kwenda kwa nchi zingine duniani.

No comments