Ads

MWENYEKITI MTAA WA ULONGONI AFUNGUKA MIPANGO UTEKELEZAJI UJENZI WA OFISI

 

Mwenyekiti wa Serikali za Mtaa Kata ya Ulongoni (A), Ukonga jiji la Ilala, Bw. Abdulrahm Munisi akizungumza jambo na waandishi wa habari katika Mkoa wa Dar es Salaam.

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam.

Mwenyekiti wa Serikali za Mtaa Kata ya Ulongoni (A), Ukonga jiji la  Ilala, Mkoa wa  Dar es Salaam Bw. Abdulrahm Munisi amesema kupitia uongozi wake amefanikiwa kutekeleza majukumu yake kwa kupambana changamoto zilizopo kwenye kata hiyo.

Mwenyekiti huyo ambaye hadi hivi sasa ana miaka miwili kwenye uongozi na tayari ameanza ujenzi wa ofisi ya kata na kwa sasa wanafanya shughuli zao kwenye ofisi ya kupanga.

Akizungumzia ujenzi wa ofisi ya kata Bw. Abdulrahm Munisi amesema kuwa ofisi hiyo ina unachumba cha ukumbi na ofisi ya mtendaji  ambayo inastoo ndogo.

"Kata yetu hii ina muda mrefu tangu 2009 haijaweza kuwa na Ofisi yake, hivyo naitaji kukamilisha ujenzi ili kata iweze na ofisi yake," amesema Munisi.

Amesema kuwa kupitia mradi wa songasi kuwepo katika kata hiyo, ndicho kimekuwa chanzo cha kupata pesa kidogo wanazolipwa kutokana na kata hiyo, kuwa walinzi wa mradi huo.

Amesema kuwa wanaunga mkono juhudi za serikali kwa kuweza kuwajenga madarasa mawili ya shule ya msingi Ulongoni A, ambapo januari 17 wameanza kutumika baada ya shule zote nchini kufunguliwa.

Amefafanua kuwa kutokana na kata hiyo haina chanzo  kingine cha mapato wamemkumbusha Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam, Bw. Jumanne Shauri kwani mwa mwaka jana walimwandikia barua.

katika kuendeleza maendeleo ya Ulongoni A eneo inapojengwa ofisi hiyo inayoitaji mwendelezo kukamilika lilitolewa na mkazi wa eneo hilo mwaka 2009.

Uongozi wa kata hiyo kupitia kwa Mtendaji kata Jenifa Shayo  wametaja kukamilika kwa majukumu mbalimbali kwa kupambana na utatuzi wa changamoto wanazokuwa nazo wananchi. 

No comments