UKWELI KUHUSU CHANZO CHA UGONJWA WA KIFAFA.
Na
Mwandishi wetu, Dar es Salaam.
Imeelezwa
kuwa baadhi ya wagonjwa wa kifafa hutokana na ajali hivyo waendesha boda boda
nchini wametakiwa kuwa makini kipindi wanapokuwa wanaendesha Ili kuzuia ajali
za mara kwa mara barabarani
Hayo yamesemwa Dkt. Bingwa
wa Magonjwa ya kifafa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili Dkt. Patience Luoga,
amesema katika hali hiyo kifafa kinasababishwa
na degedege ambapo wagonjwa wenge wametajwa kuanzia umri wa wastani miaka 15 na
zaidi ya asilimia 25 ya wagonjwa wa kifafa Wana ulemavi .
"Hali ya ulemavu huo
husababishwa na kuanguka wakati wa ugonjwa anapopata degedege na nchini
Tanzania zaidi ya watu milioni moja
wanaugonjwa wa kifafa,"anasema Dkt Luoga.
Dkt. Luoga amesema kwa
kuwa watajwa hapo wengi ni wenye wastani miaka 15 ndio hasa takwimu zinaonesha
hivyo na kwakua boda boda wengi ni
vijana na amewaasa kujilinda kutokupata ajali za barabarani ilikuja kuepukana
na matatizo ya kupata kifafa pindi wapatapo ajari.
Aidha amesema visa vya
bodaboda ni vingi vya wanaofika kupatiwa matibabu katika Hospitali hiyo ya Taifa ya Muhimbili .
Aliendelea kueleza kuwa
watu wanaoishi na kifafa no zaidi ya watu 60 milioni Duniani kote na niongezeko
la watu 34 Hadi 76 kwa watu 200000 kwa mwaka.
Serikali kutoa elimu
vijijini na utoaji dawa za kutosha kutibu wagonjwa hao , hali inayoweza
kupunguza kiwango cha ugonjwa wa kifafa huku zaidi ya asilimia 25 ya wagonjwa
wa kifafa wakitajwa wanaulemavu unaosababishwa na kuanguka wakati wa ugonjwa
kutokana na kupata degedege.
Madaktari wa Muhimbili
wataadhimisha siku hiyo ambayo itafanyika Februari 14 mwaka huu
kwa kutoa elimu kwa jamii .
Chama Cha Wagonjwa wa
Kifafa nchini (TEA), kuelekea siku hiyo kimeweza kuzunguza na wananchi kwa
kutumia vyombo vya habari , kwamba ugonjwa huo unatibika na hivyo kuacha imani za kishirikina na badala yake
kimewataka kuwapeleka wagonjwa hospitali mapema.
“Wengi wana imani potofu
kwamba mtu mwenye kifafa, kimesababishwa na mashetani, lakini si kweli
kwani wanasayansi walibaini kuwa
mshutuko wa ubongo ndio unasababisha kifafa kutokana na sababu mbalimbali,”
amesema Dkt.Luoga.
Hospitali ya Taifa
Muhimbili mara zote imekuwa ikipambanua kua, mtu anapata kifafa wakati
anapozaliwa endapo ataumia sehemu ya kichwani, kukosa hewa au mtoto kuumizwa
kichwani kua atapata degedege.
Post a Comment