Ads

AGIZO LA KATIBU MKUU WIZARA YA MALIASILI NA UTALII KUHUSU MATUMIZI YA FEDHA KUBORESHA KIJIJI CHA MAKUMBUSHO

Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. France Michael amewaagiza watendakazi wa Makumbusho ya Taifa kuhakikisha  kiasi cha fedha shilingi milioni miambili na moja  zilizotengwa  na Mhe Raisi Samia Suluhu za miradi zinatumika kwa mlengo uliokusudiwa.

Agizo hilo amelitoa leo Jijini Dar es salaam katika Uzinduzi wa Uboreshaji wa Kijiji Cha Makumbusho Kukuza Utalii wa Kiutamaduni kupitia mpango wa maendeleo kwa ustawi wa Taifa na mapambano dhidi ya Uvico 19 ambapo amesema fedha hizo zitasaidia kujenga nyumba za asili ya makabila mbalimbali ikiwemo wazanaki ili kuendelea kulinda utamaduni wao.

Sanjari na hayo Dkt. Michael amesema fedha hizo zitajenga nyumba za asili za makabila mbalimbali ikiwemo Wazanaki ili kusaidia kuhifadhi vitu vya asili na nyaraka zao na kuvutia watalii ndani na nje  na zitafanya maboresho katika vituo vyote ili kusaidia kuvutia Utalii wa kiutamaduni na kuongezeka watalii  na watafiti kufanya tafiti zao na itakua chachu kuvutia watalii wengi na pato la Taifa kuongezeka..

"Miradi hii imezinduliwa kutokana na fedha hizo nakuwa ni matarajio  zitakwenda kukuza utalii na unategemea kubadirisha taswira ya makumbusho,"amesema Dkt. Michael.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Makumbusho ya Taifa Dkt. Noeli Luoga amemshukuru Raisi kwa jitihada kubwa kusaidia kuboresha miundombinu na vituo vya utalii Nchini na kukuza Uchumi wa Taifa

No comments