Ads

SHUHUDA TUKIO LA MLIPUKO WA MABOMU UGANDA ASIMULIA MKASA MZIMA

Kufuatia tukio hilo  , Naibu spika wa Bunge nchini Uganda  , Anita Among amesitisha shughuli za Bunge na kuwataka wabunge kubaki majumbani wakati hali ya usalama ikiwa tete katika jiji la Kampala kufuatia milipuko miwili.
Uamuzi huo umetolewa dakika chache baada ya kutokea milipuko hiyo katika maeneo mawili tofauti leo Jumanne asubuhi.
Mlipuko wa kwanza ulitokea katikati ya jiji na dakika chache baadaye mwingine ulilipuka katika barabara ya Bunge na kugonga jengo la bima la Jubilee ambalo pia lina ofisi za mkaguzi mkuu wa ofisi za Serikali.
Watu wengi wanadaiwa kufariki na wengine kadhaa kujeruhiwa katika milipuko hiyo huku Wabunge na watumishi wengine wa Bunge wametakiwa kubaki nyumbani.

No comments