Ads

BREAKING NEWS ; MLIPUKO MKUBWA KITUO KIKUU CHA POLISI NA BUNGE NCHINI U...


Mabomu mawili yamelipuka leo katika Jiji la Kampala nchini Uganda.

Taarifa kutoka Kampala zinasema kuwa bomu moja limelipuka mkabala na Kituo Kikuu cha Polisi katika Jiji la Kampala lingine likilipuka karibu na jengo la Bunge la Nchi hiyo.

Kutokana na milipuko hiyo, Bunge la Uganda limezingirwa na vyombo vya ulinzi na usalama.
Kwa mujibu wa vyombo vya habari nchini humo, baadhi ya watu wamejeruhiwa kutokana na milipuko hiyo.

Picha na video ambazo zimesambaa kwenye mitandao ya kijamii zinaonyesha moshi mzito umetanda huku baadhi ya magari yakionekana yakiwa yanateketea kwa moto.

No comments