Ads

Maelfu ya raia wa Ethiopia wameandamana kuiunga mkono serikali.

 


Maelfu ya raia wa Ethiopia wameandamana jana kuiunga mkono serikali ya Waziri Mkuu Abiy Ahmed, wakati vikosi vya serikali vikiwa vinapambana na makundi ya waasi wanaotishia kuingia kwenye mji mkuu wa Addis Ababa. 

Baadhi ya waandamanaji wameilaani Marekani, baada ya serikali ya Rais Joe Biden kuishutumu Ethiopia Jumanne kwa ukiukaji mkubwa wa haki za binadamu, na kuonya kwamba inapanga kusitisha biashara na nchi hiyo. 

Marekani ni mojawapo ya nchi za kigeni zilizotoa wito wa kusitishwa mapigano hayo yaliyodumu kwa mwkaa mmoja, na ambayo yamezidi kushika kasi wiki za hivi karibuni. 

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, Umoja wa Afrika, Kenya na Uganda pia wametoa wito wa kusitishwa kwa mapigano ya mzozo huo uliosababisha vifo vya maelfu ya watu.

chanzo DW

No comments