GLOBAL PEACE FOUNDATION TANZANIA YAWAKUTANISHA WADAU KUCHAMBUA MATOKEO YA UTAFITI WA UKATILI WA KIJINSIA SOKA LA WANAWAKE.
Mwakilishi wa Mfuko wa Wanawake Tanzania (WFT Trust) Bi. Bernadetha kafuko akizungumza jambo jijini Dar es Salaam katika Mdahalo wa Kitaifa wa kuchambua utafiti juu ya Ukatili wa kijinsia katika mpira wa miguu kwa wanawake uliondaliwa na Taasisi ya Global Peace Foundation Tanzania kwa kushirikiana na Chama cha Mpira wa Miguu wa Wanawake Tanzania (TWFA) chini ya ufadhili wa Mfuko wa Wanawake Tanzania (Women Fund Tanzania Trust).
Katibu wa Chama Cha Mpira wa Miguu Wanawake Tanzania (TWFA) Bi. Somoe Ng’itu akizungumza jijini Dar es Salaam katika Mdahalo wa Kitaifa wa kuchambua utafiti juu ya Ukatili wa kijinsia katika mpira wa miguu kwa wanawake hapa nchini uliondaliwa na Taasisi ya Global Peace Foundation Tanzania kwa kushirikiana na Chama cha Mpira wa Miguu wa Wanawake Tanzania (TWFA) chini ya ufadhili wa Mfuko wa Wanawake Tanzania (Women Fund Tanzania Trust)
Meneja wa Mradi, Ufuatiliaji na Tathmini kutoka Grobal Peace Foundation Bi. Irene Ishengoma akizungumza jijini Dar es Salaam katika Mdahalo wa Kitaifa wa kuchambua utafiti juu ya Ukatili wa kijinsia katika mpira wa miguu kwa wanawake hapa nchini uliondaliwa na Taasisi ya Global Peace Foundation Tanzania kwa kushirikiana na Chama cha Mpira wa Miguu wa Wanawake Tanzania (TWFA) chini ya ufadhili wa Mfuko wa Wanawake Tanzania (Women Fund Tanzania Trust)
Muongoza Mdahalo ambaye ni Afisa Mradi wa UN Women Bi.
Agnes Hanti akitoa ufafanuzi wa jambo katika
Mdahalo wa Kitaifa wa kuchambua utafiti juu ya Ukatili wa kijinsia katika mpira
wa miguu kwa wanawake hapa nchini uliondaliwa Taasisi ya Global Peace Foundation Tanzania kwa kushirikiana na Chama cha Mpira wa Miguu wa Wanawake Tanzania (TWFA) chini ya ufadhili wa Mfuko wa Wanawake Tanzania (Women Fund Tanzania Trust)
Kiongozi wa kamati ya amani viongozi wa dini Mkoa wa
Dar es Salaam Mchungaji Christosiler Kalata akichangia mada jijini Dar es
Salaam katika Mdahalo wa Kitaifa wa kuchambua utafiti juu ya Ukatili wa
kijinsia katika mpira wa miguu kwa wanawake hapa nchini uliondaliwa Taasisi ya Global Peace Foundation Tanzania kwa kushirikiana na Chama cha Mpira wa Miguu wa Wanawake Tanzania (TWFA) chini ya ufadhili wa Mfuko wa Wanawake Tanzania (Women Fund Tanzania Trust)
Mtafiti kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) Dkt.
M. Lucius akitoa ufafanuzi wa utafiti juu ya Ukatili wa kijinsia katika mpira
wa miguu kwa wanawake hapa nchini.
Baadhi ya washiriki wakiwa katika Mdahalo wa Kitaifa wa
kuchambua utafiti juu ya Ukatili wa kijinsia katika mpira wa miguu kwa wanawake
hapa nchini uliondaliwa na Taasisi ya Global Peace Foundation Tanzania kwa kushirikiana na Chama cha Mpira wa Miguu wa Wanawake Tanzania (TWFA) chini ya ufadhili wa Mfuko wa Wanawake Tanzania (Women Fund Tanzania Trust).
NA NOEL RUKANUGA, DAR ES
SALAAM.
Taasisi mbalimbali kwa
kushirikiana na wadau wa michezo wametakiwa kupinga ukatili wa kijinsia katika
mchezo wa mpira wa miguu wa wanawake ikiwemo rushwa ya ngono jambo ambalo litasaidia
kupiga hatua katika nyanja za kimaendeleo.
Hatua hiyo imekuja baada
ya Taasisi ya Global Peace Foundation Tanzania kwa kushirikiana na Chama cha
Mpira wa Miguu wa Wanawake Tanzania (TWFA) chini ya ufadhili wa Mfuko wa
Wanawake Tanzania (Women Fund Tanzania Trust) kufanya utafiti juu ya masuala ya
Ukatili wa Kijinsia katika soka la wanawake.
Utafiti huo umeonesha
asilimia kubwa kuna ukatili wa kijinsia unaofanywa na watu mbalimbali wakiwemo baadhi
ya wanajamii, viongozi/wasimamizi wa soka (vilabu, taasisi zinazojihusisha na
soka), hata wachezaji wenyewe aidha kwa kujua ama kutokujua.
Mfuko wa Wanawake Tanzania
(Women Fund Tanzania Trust)chini ya uongozi imara wa Mkurugenzi Mtendaji, Mama
Mary Rusimbi umekuwa mstari wa mbele kufadhili miradi mbalimbali inayolenga
kuwawezesha ama kuwajengea uwezo wanawake kugundua talanta na uwezo walionao
ndani yao ili wanawake hao wawe sehemu ya mabadiliko chanya katika jamii.
Maono haya ndio
yaliwavutia kufadhili utafiti huu ambao lengo lake kuu ni kutokomeza aina zote
za ukatili katika mpira wa miguu hasa mpira wa miguu wa wanawake na kuwajengea
uwezo wanawake hao kushiriki soka kimafanikio Zaidi.
Akizungumza jijini Dar es
Salaam Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Michezo Bw. Alex Makoye Nkenyenge katika “Mdahalo
wa Kitaifa wa kuchambua matokeo utafiti juu ya Ukatili wa kijinsia katika mpira
wa miguu wa Wanawake hapa nchini” uliondaliwa na Taasisi ya Global Peace
Foundation Tanzania kwa kushirikiana na Chama cha Mpira wa Miguu wa Wanawake
Tanzania (TWFA) chini ya ufadhili wa Mfuko wa Wanawake Tanzania (Women Fund
Tanzania Trust).
Ukiendeshwa na Bi. Agnes
Hanti, Afisa mradi wa maswala ya jinsia kutoka UN women Tanzania, ambao
wamekuwa mstari wa mbele kushirikiana na Global Peace Foundation Tanzania
katika kupinga ukatili wa kijinsia katika mpira wa miguu kwa wanawake.
Bw. Nkenyenge amesema kwa
sasa kila mmoja anatakiwa kujikita katika kuondoa kiini cha tatizo ili vijana
wanawake wapate fursa ya kushiriki mpira wa miguu kwa furaha na amani kwani
michezo ni afya na ajira.
Bw. Nkenyenge alikuwa
mgeni rasmi katika Mdahalo huo akimwakilisha “Mh. Paulina Gekul Naibu Waziri,
Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo”, ameeleza kuwa upo unyanyasaji katika
soka la wanawake kwani baadhi ya wazazi wamekuwa na tabia ya kuwazui watoto wa
kike wasicheze mpira wa miguu.
“Kupitia matokeo ya utafiti
na mdahalo huu utatusaidia kupata vitu vizuri ambavyo tutavipeleka katika jamii
ili kupata mtazamo mpya ambao utakuwa rafiki katika kulisaidia soka la wanawake
kuendelea kupiga hatua” amesema Bw. Nkenyenge.
Amefafanua kuwa serikali
inaendelea kutoa ushirikiano katika soka la wanawake kutokana bado wanamchango
mkubwa katika michezo, kwani kumbukumbu zinaonyesha mwaka 1965 mwanamke ndiye
alikuwa wa kwanza kuleta medani hapa nchini.
Bw. Nkenyenge ametoa wito
kwa wadau mbalimbali kufanyia kazi utafiti huo ambao umeonesha changamoto nyingi
katika soka la wanawake hapa nchini.
Mkurugenzi wa Taasisi ya
Global Peace Foundation Tanzania Bi. Martha Nghambi, amesema kuwa wameamua
kufanya utafiti katika mchezo wa mpira wa miguu wa wanawake ili kuwasaidia
waweze kushiriki kwa amani.
Bi. Nghambi amesema kuwa
utafiti umefanyika ili kujua kiwango cha ukatili wa kijinsia katika soka la
wanawake upo kwa kiasi gani mpaka sasa, kujua mapungufu ya kisera, sheria
ndogondogo na miongozo mbalimbali inayoshughulikia masuala ya ukatili katika
soka na kuona namna ya kushirikisha wadau wa michezo kwa pamoja kuona namna ya
kulitatua tatizo hili kwa maendeleo la soka la Wanawake Tanzania.
Amebainisha kuwa utafiti
huo umefanyika katika Mikoa ya Dar es Salaam, Dodoma na Zanzibar kwa kushirikiana
na wadau mbalimbali wa michezo,”Matokeo kamili ya utafiti huu tutayatoa hivi
karibuni kupitia vyombo vya habari na sehemu mbalimbali ili umma waweze kujua kuna
ukatili wa jinsia katika sekta ya michezo na waweze kuongeza nguvu katika kupinga
ukatili huo” amesema Bi. Nghambi.
Meneja wa Mradi, Ufuatiliaji
na Tathmini kutoka Global Peace Foundation Tanzania Bi. Irene Ishengoma, amesema kuwa “mchezo wa soka kiasili
na kiutamaduni unachukuliwa kama mchezo wa kiume, hivyo hata mafanikio ya
mchezo huo yanaangaliwa zaidi hata kupewa kipaumbele na kufatiliwa kwao tofauti
na wanawake.
Bi. Ishengoma ameeleza
kuwa baadhi ya watu wanaamini mwanamke akicheza soka ni kinyume na taratibu na
maadili ya kitanzania (uhuni), jambo ambalo linasababisha kikwazo kwa wanawake
wengi kushiriki kucheza mpira wa miguu huku wakisahau kuwa soka la Wanawake ni
jukwaa la kupaza sauti na kuonesha kuwa Wanawake wanaweza.
“Soka kwa sasa ni fursa
kwa kila mtu, ni mahali sahihi kwa mwanamke au msichana kushiriki na kupata
mafanikio, hivyo kupitia mradi huu kuna umuhimu wa kuendelea kutoa elimu kwa
jamii na wachezaji juu ya fursa za ajira/kipato katika sekta ya michezo”
amesema Bi. Ishengoma.
Pia, Bi. Ishengoma ameshukuru
Wizara ya Michezo, Mashirikisho ya Mpira wa Miguu Tanzania bara na visiwani
(TFF na ZFF), Baraza la Michezo la Taifa Tanzania bara na visiwani (BMT na
BTMZ), Viongozi wa dini, Vyombo vya Habari, viongozi na wachezaji wa vilabu
mbalimbali pamoja na wadau mbalimbali wa michezo waliofanikisha zoezi la
ukusanyaji data kwa asilimia kubwa.
Mtafiti kutoka Chuo Kikuu
cha Dar es Salaam (UDSM) Dkt. M. Lucius, ametoa wito kwa taasisi mbalimbali
kuweka mkazo katika kuboresha miongozo na kusimamia soka la wanawake hapa
nchini.
Mwakilishi wa Mfuko wa
Wanawake Tanzania (WFT Trust) Bi. Bernadetha kafuko, amesema kuwa michezo ni
afya, ajira hivyo wanawake wengi wanatamani kupata fursa kupitia vipaji vyao.
Amesema kuwa rushwa ya
ngono inamfanya mwanamke kushindwa kushiriki michezo kwa ajili ya kuonesha
kipaji chake cha mpira wa miguu.
“Natamani kuona Shirikisho
la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) wanalisimamia hilo, pia katika kamati zao za
kufanya maamuzi wanakuwepo wakinamama” amesema Bi. Kafuko.
Katibu wa Chama Cha Mpira
wa Miguu Wanawake Tanzania (TWFA) Bi. Somoe Ng’itu, amesema kuwa mchezo wa
mpira wa miguu kwa wanawake upo na wanaendelea kushiriki ligi mbalimbali kama
ilivyo kwa wanaume.
Ameeleza kuwa mpira wa
miguu kwa sasa ni ajira na wanawake wengi wamekuwa wakishiriki katika nafasi
mbalimbali za soka ikiwemo kusimamia wakiwemo waamuzi na wanaendelea kufanya
vizuri.
“Tunajivunia kuona soka la
wanawake linachezwa katika ngazi zile zile kama wanaume wanavyocheza, mpira ni
ajira, ni taaluma” amesema Bi. Ng’itu.
Kwa upande wake Mwakilishi
wa Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) Bw. Boniphance Wambura
amesema kuwa watajitahidi kuyafanyia kazi mawasilisho hasa changamoto zote
zilizoonekana katika soka la wanawake.
Bw. Wambura amebainisha
kuwa TFF wanasubiri ripoti hiyo ya utafiti katika soka la wanawake kwa ajili ya
kuzifanyia kazi changamoto zote zilizoonekana.
Huku Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Zanzibar (ZFF) Bw. Abdullatif A. Yassin akisisitiza “suala la Wanawake na wasichana wenye vipaji kucheza soka huku wakibakia na uasilia wao wa uanamke ndani na nje ya uwanja”.
Post a Comment