DC Ludigija ampongeza Rais Samia kwa kuipatia Ilala Fedha za Sekta ya Elimu

Mkuu wa Wilaya ya Ilala Ng’wilabuzu Ludigija amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzamia Samia Hassan Suluhu, kuwapatia shilingi Bilioni 5.1 fedha kwa ajili ya ujenzi wa madarasa idara ya Elimu Sekondari madarasa 255
Mkuu wa Wilaya Ludigija ametoa pongezi hizo katika ziara yake na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya Ilala, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji, Meya wa Halmashauri hiyo na Wataalam, katika kufatilia ujenzi huo .
“Nampongeza Rais wetu kuwekeza katika sekta ya Elimu ametupatia fedha za kutosha shilingi Bilioni 5.1 kwa ajili ya ujenzi wa madarasa ya UVIKO -19 ujenzi unaendelea vizuri tutasimamia fedha hizi kufanikisha ujenzi wa madarasa 255 “alisema Ludigija
Amesema ziara hiyo ni endelevu kukagua madarasa ya shule za zote za Halmashauri ya jiji la Dar es Salaam lenye shule 41 jana amefanikiwa kukagua shule kumi kati 41 ambazo zinajengwa madarasa ya UVIKO 19.

Mkuu wa Wilaya Ludigija ameridhishwa na kasi ya ujenzi wa vyumba hivyo vya madarasa kwa baadhi ya shule alizozitembelea huku akisema ziara hiyo ni endelevu akitoa pongezi kwa wasimamizi wa ujenzi wa shule hizo Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam Jumanne Shauri, Meya wa Halmshauri ya Jiji Mhe. Omary Kumbilamoto na Watendaji wake wa Idara ya Elimu Sekondari pamoja na kamati za Ujenzi za Shule na Walimu wote .
“Nichukue nafasi hii kuwapongeza walimu, kamati zote za shule za ujenzi kwa kazi kubwa ambayo nimeiona imefanyika kwa maeneo ambayo nimetembelea, lakini wito wetu sisi kama Wilaya na kama ambavyo Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan amesema fedha hizi zisimamiwe vizuri na kuleta tija tunamuahidi kutekeleza maelekezo yake kwa weledi na tunataka tuone ujenzi huu unakamilika kwa wakati lakini kwa kuzingatia ubora” alisema
Post a Comment