Ads

SIMBA YAJA NA KAULIMBIU YA ‘IS NOT OVER, KAZI IENDELEE’ MAHSUSI KWA KUWA VAA JWANENG GALAXY FC.



Na Bakari Madjeshi

WAWAKILISHI pekee wa nchi katika Michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika, Simba SC Oktoba 24, 2021 wanarejea nyumbani Benjamin Mkapa, Dar es Salaam kuwaalika timu ya Jwaneng Galaxy FC ya Botswana katika mchezo wa mkondo wa pili wa Michuano hiyo

Simba SC inaingia katika mchezo huo ikiwa na kumbukumbu ya ushindi wa bao 2-0 dhidi ya timu hiyo katika mchezo uliopigwa Oktoba 17, 2021 katika dimba la Gaborone nchini humo, Simba SC ilipata ushindi huo kwa mabao ya Mshambuliaji, Nahodha John Raphael Bocco katika dakika za mapema.

Akizungumza kuelekea mtanange huo, Maidizi wa Afisa Habari wa Klabu hiyo, Ally Shatry amesema maandalizi yamekamilika kwa 80%, amesema Wachezaji wote wana ari na molali ya hali ya juu kuwakabili Jwaneng Galaxy FC siku ya Jumapili.

“Wapinzani wetu, Jwaneng Galaxy wameingia nchini jana na sisi Wachezaji wetu wapo tayari kambini kwa ajili ya mchezo wetu muhimu ambao tukishinda tunafuzu Makundi. Tunaingia na Kaulimbiu ya ‘IS NOT OVER KAZI IENDELEE’ kuhakikisha tunashinda mchezo huo”, amesema Shanty 

Kwa upande wake, Mhamasishaji wa timu hiyo, Mwijaku amesema wanaamini watashinda kutokana na maandalizi kabambe ya Kikosi chao cha Simba SC, amesema ameongea na Nahodha Bocco ambaye amemhakikishia Wachezaji wote wapo tayari kwa mchezo na kuleta ushindi kwa Simba SC na Taifa kwa ujumla.

“Timu inaingia Benjamin Mkapa dhidi ya Jwaneng Galaxy FC tukiamini tunaenda kuwakilisha nchi katika Michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika, kwa maandalizi ya timu tunaamini tutapata ushindi na kusonga mbele hatua ya makundi ya Michuano hiyo mikubwa Afrika”, amesema Mwijaku.

Naye, Mhamasishaji K Mziwanda amesema hakuna wasiwasi kwa Simba SC  kushinda mchezo wao dhidi ya Jwaneng Galaxy FC kutokana na maandalizi yake huku ukiwa na ushindi wa bao 2-0 uliopatikana ugenini nchini Botswana, amesema timu hiyo inatoa tahadhari kwa kila anayekuja mbele yao kutokana na uzoefu waliokuwa nao wakiwa kwenye uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam.



No comments