Ads

RAIS WA ZANZIBAR DK.HUSSEIN ALI MWINYI LEO AMEWAAPISHA VIONGOZI ALIOWATEUWA

 

Rais  wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi akimuapisha Capt.Khatib Khamis Mwadini   kuwa  Naibu Mkuu wa Kikosi Maalum cha Kuzuia Magendo (KMKM) wakati wa  hafla iliyofanyika leo Ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar.[Picha na Ikulu] 21/10/2021.
Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe.Hemed Suleiman (kulia) Abdulla,Spika wa Baraza la Wawakilishi la Zanzibar Mhe.Zubeir Ali Maulid pamoja na Viongozi wengine ni miongoni mwa Viongozi waliohudhuria katika hafla ya kuapishwa Viongozi   walioteuliwa na Rais  wa Zanzibar  na Mwenyekiti wa Baraza wa Mapinduzi   Dk.Hussein Ali Mwinyi hivi karibuni  katika hafla  iliyofanyika leo Ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar.
Rais  wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi (kushoto) akiwa amesimama na Viongozi wengine wakati Wimbo wa Taifa ukipigwa na Kikundi cha Brass Band  cha  Jeshi la Polisi katika hafla ya kuapishwa Viongozi   aliowateuwa hivi karibu kushika nafasi mbali mbali za Uongozi hafla  iliyofanyika leo Ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar.
Viongozi walioteuliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza a Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi wakiangalia hati za Viapo vyao kabla kuapishwa rasmi katika hafla  iliyofanyika leo Ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar.
Rais  wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi akimuapisha Balozi Masoud Abdalla Balozi  kuwa Katibu wa Rais wa zanzibar -Ofisi ya Rais - Ikulu   hafla iliyofanyika leo Ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar.
Rais  wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi akimuapisha Bw.Suleiman Abdulla Salum  kuwa Katibu wa Tume ya Utangazaji hafla iliyofanyika leo Ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar.
[Picha na Ikulu] 21/10/2021.

No comments