SERIKALI YAPONGEZWA KUWAONDOA MACHINGA MBELE YA MADUKA YA WAFANYABIASHARA
Na Francisco Peter -Dar es salaam
Jumuiya ya wafanyabiashara Tanzania (JWT) imempongeza
serikali Kwa kuagiza Wamachinga kote nchini waondokebele ya maduka ya
wafanyabiashara walio rasmi wanaofuta taratibu za kuendesha shughuli zao za
kibiashara
Pombezi hizo amezitoa karibu mkuu wa jumiya ya
wafanyabiashara Tanzania (JWT) Abdallah Mwinyi ambapo amesema miaka michache
iliyopita ulijitokeza mpangilio holela wa kufanya Biashara popote Kwa muda
mrefu Hali ambayo ilifilisi wafanyabiasha wengi walio rasmi hadi wengine kuamua
kutumia njia mbadala ya kufanya Biashara Kwa kuwatumia hao hao machinga kuuza
bidhaa zao
"Huu ni ukombozi mpya Kwa wafanyabiashara Rais wa Jamuhuri ya Muungano Tanzania Mh:
Samia Suluhu Hassan na Serikali yake kwa ujumla Kwa kuagiza Wamachinga wote
waondoke mbele ya maduka na makusanyo ya Kodi kwa Taifa kwani tunatambua kuna
wafanyabiashara walitumia kitambulisho cha mmachinga kama kichaka cha kukwepa
kulipa kodi"alisema Mwinyi
Mkurugenzi wa mahusiano jumuiya ya wafanyabiashara
Tanzania Stephen Chamle ameiomba serikali kufanya utafiti wa kutosha katika
masoko yote kumbaini machinga kwa kuwawekea utaratibu namba ya kufanya biashara
ili kuepusha migogoro kwani wote wanategemeana.
Hata hivyo jumuiya hiyo ya wafanyabiashara wameiyomba
serikali kushirikishwa kwa kutoa maoni yao katika uwekezaji Mradi mkubwa unaotarajiwa kufanyika Ubungo
Kwa ujenzi wa kituo kikubwa cha Biashara kinachotarajiwa kuwa na maduka zaidi
ya elfu tatu(3000)
Jumuiya hiyo imesema ushauri wao kabla ya Mradi huo kufanyika ni vyema kongamano kubwa lifanyike la uhuru wa maoni kwa wadau na no waagizaji bidhaa kutoka nje ya Nchi ili kuepusha watanzania kuwa watumwa wa biashara kwenye soko la ndani.
Post a Comment