RAIS SAMIA APONGEZWA KUENZI UTAMADUNI WA ASILI .
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja
(Mb) amempongezza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuenzi utamaduni
ikiwa ni pamoja na utamaduni wa ngoma za asili kwa sababu Serikali yake ya
Awamu ya Sita inatambua matamasha hayo.
Akizungumza na wananchi leo katika Tamasha la Ngoma za
Asili lijulikanalo kama Tulia Traditional Dances lililofanyika leo katika
Viwanja vya Airport ya zamani jijini Mbeya.Mhe. Masanja amefafanua kuwa, Sekta
ya Utalii inatambua kwa asilia mia kwamba utamaduni wa ngoma za asili ni sehemu
mojawapo ya kuhamasisha utalii na pia unasaidia kuongeza pato la Taifa na pato
la mwananchi mmoja mmoja.
Amewahamasisha wananchi kuendelea kuandaa matamasha
kama hayo kwa kila kanda ili mwisho wa siku yavutie wageni
kutoka nje ya nchi waje kuangalia utamaduni huo.
Mhe. Masanja amepongeza Naibu Spika wa Bunge, Dkt.
Tulia Ackson kwa kurudisha tamasha la Utamaduni wa ngoma.
Post a Comment