SERIKALI, JAMII INATAKIWA KUONGEZA JUHUDI KUTOKOMEZA NDOA ZA UTOTONI.
Mtandao wa kutokomeza ndoa za utotoni Tanzania (TECMN) umeiomba
serikali,jamii na wadau wote wa maendeleo kuongeza juhudi za pamoja kuhakikisha
suala la ndoa za utotoni linatokomezwa ili kusaidia kujenga kizazi kijacho
chenye usawa wa kiuchumi.
Ombi hilo limetolea Jijini Dar es salaam na Mratibu Mtandao wa kutokomeza ndoa za utotoni Euphomia Edward katika kikao kazi kilichojumuisha Mashirika yasiyo ya kiserikali 64 ambapo amesema kwa mujibu wa takwimu kutoka utafiti wa Demografiana afya Tanzania wa mwaka 2015/2016 zinaonyesha asilimia 36 ya wasichana wenye umri kati ya miaka 20_24 waliolewa kabla ya kutimiza umri wa miaka 18.
Mwakilishi kutoka Shinyanga Mstapha Sebuja amesema ndoa za utotoni husababishwa na umasikini,mila potofu, desturi,ukosefu wa elimu ,mapungufu katika sheria ya ndoa ya mwaka 1971 sheria hii wadau na serikali wangekaa na kuifanyiia marekebisho
"Ni kweli kabisa mkoa wa Shinyanga ndio mkoa unaoongoza Kwa ndoa za utotoni kwa asilimia 59 ukifuatiwa na Tabora asilimia 58 Mara asilimia 55 huku Dodoma ukiwa asilimia 51 hali hii ya mikoa hii ni hatari sana kwa watoto wa kike wanaotokea katika jamii hizi ni budi serikali na wadau wengine kuongeza jitihada za makusudi kutokomeza suala hili"alisema Sebuja
Mwakilishi kutoka Tabora Mayaya Marko amesema watoto wa kike wanaolewa kabla ya umri wa miaka 18 wanakumbana na changamoto ya kupoteza fursa ya elimu,kupata maambukizi ya virusi vya ukimwi na magonjwa ya zinaa,kuteseka kisaikolojia ,kuyumba kiuchumi,kuwa katika hatari kubwa kufanyiwa unyanyasaji wa kijinsia
Wito umetolewa kwa watu watu wote kutoa ushirikiano Kwa vyombo vya sheria pale wanapoona viashiria vya kuozeshwa mtoto wa kike aliye chini ya umri wa miaka 18.
Post a Comment