Ads

JBI YAFANYA MAHAFALI 19

 Chuo cha Japan Bible Institute (JBI)ambacho kinatambulika duniani kote, kilifanya mahafali yake ya 19 ambapo kiliweza kutoa shahada mbalimbali huku miongoni mwa waliopewa shahada ya Heshima (Dr .Of Humanity) akiwa Dr.Albert Katagira  Mkurugenzi wa Tusiime Sekondari iliyopo Tabata, Ilala Jijini Dar es Salaam.

Mgeni rasmi katika mahafari hayo yaliyofanyika mwisho wa wiki katika viwanja vya Karimjee , Meya wa Jiji la Dar es Salaam Omary Kumbilamoto amesema kuwa kufanyika kwa mahafari hayo kunaongeza tija katika jamii kwani mafunzo waliopata yapo katika nyanja mbali mbalimbali katika masuala ya dini  na jamii.

"Tunaamini kuwa shahada walizozipata zitakwenda kuchochea mafanikio yao pamoja na serikali kupata faida kwa kuwa kupitia masomo yao ambayo yataleta faida katika kuifanya jamii kustawi,"amesema. 

Mkuu wa Mafunzo Bishop Dr Bartholomew Sheggah amesema kuwa amewapatia shahada ya Udaktari wa heshima Mkurugenzi Dkt.Katagira  ambapo imetokana na mchango  anaotoa katika masuala ya kijamii.

Bishop Dr Bartholomew ambaye pia ni Makamu Mkuu wa Chuo cha JBI  amesema moja ya mambo wanayo fundishwa kupitia chuo hicho ni  imani .

"Tunawafundisha ili watakapotoka katika kuitumikia jamii  na waumini na mbele za serikali wakaonekane kuwa waaminifu , weledi , mahiri kama neno la Mungu linavyo sema katika Timotheo 2:15," amesema Bishop Bartholomew.

Amesema Timotheo 2:15 imesema "Jitaidi kujionyesha kuwa umekubaliwa na Mungu  mtenda kazi , asiye na sababu ya kutahayari ukitumia neno la kweli wa halali".

Katika siku hiyo vile vile mwingne aliyepata Udaktari wa heshima alikuwa ni Dr.Mery ambaye ameelezewa kuwa ni mmoja ya watu wenye kusaidia kujitoa kustawisha jamii jwa kufanya mambo mengi ya muhimu.

"Ilikua sirahisi kupata kutunukiwa Udaktari huo alio pata , alifikiria siku nyingi sana ila nifuraha ya kipekee kwani kira mara alikuwa akiota juu ya lini ataweza kukupata, ila kwa sasa anakwenda kuutendea haki,"amesema Dkt. Katagira.

Tusiime limekuwa ni jina lenye umaarufu kutokana na kuwepo na msaada kwenye jamii inajipambanua katika hali kuu zifuatazo Tusiime Schools, Tusiime kupitia Nursery School, Primary Schools pamoja na Sekondary Schools.

No comments