SERIKALI YAKUTANA NA VIJANA KUJADILI RASIMU YA SERA YA TAIFA YA MAENDELEO.
Baadhi ya vijana
walioshiriki Kikao cha Kujadili na Kuthibitisha Rasimu ya Sera ya Taifa ya
Maendeleo ya Vijana wakifuatilia hotuba ya mgeni rasmi
Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Vijana Ofisi ya Waziri Mkuu Bw.Julius
Tweneshe akisoma hotuba kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Ofisi hiyo wakati wa kikao
cha Vijana cha Kupitia na Kuthibitisha Rasimu ya Sera ya Taifa ya Maendeleo ya
Vijana hii leo Jijini Dar es Salaam.
........................
Francis Peter, Dar es Salaam.
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imekutana na kundi la vijana kutoka mikoa tofauti kwa ajili ya kujadili Rasimu ya Sera ya Taifa ya Maendeleo ya Vijana.
Imeelezwa kuwa serikali imekusudia kulisaidia kundi la vijana linakuwa katika Mazingira bora na endelevu kupitia Sera ya Taifa ya Maendeleo ya Vijana inayoandaliwa kupitia Rasimu ya Sera hiyo inayoshirikisha na inayopendekezwa na vijana hao wa kada mbalimbali.
Akizungumza leo jijini Dar es Salaam na vijana wa mikoa ya Dar, Lindi, Mtwara, Pwani na Tanga, Ofisa Maendeleo ya Vijana Mkuu kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Bw. Julius Tweneshe katika Kikao cha kujadili Rasimu ya Sera ya Taifa ya Maendeleo ya Vijana ambapo ameeleza mipango mbalimbali.
Tweneshe amesema lengo kuu la kukutana na Vijana hao ilikuwa kujadili masuala mbalimbali sambamba na taifa zima yakiwemo masuala ya Uchumi, Afya, Uwezeshwaji Kiuchumi, Ubunifu, masuala ya Diplomasia, Mazingira wezeshi katika Biashara, Kilimo, Upatikanaji wa Ajira na mengineyo.
“Kuna Kamati maalum imeundwa kwa kupitia maoni ya Vijana na baadae kupata taratibu ili kuboresha Sera kwa Vijana wa Taifa lote la Tanzania. Maoni yao watayatoa kwa njia ya kuzungumza na kuwasilisha kupitia Fomu maalum iliyoandaliwa”, amesema Tweneshe.
Kwa upande wao Vijana wameomba Rasimu hiyo kufanyiwa kazi ipasavyo kwa maoni yao mazuri kuchukuliwa ili kupata Sera bora ya Maendeleo ya Taifa kwa Vijana. “Serikali kupitia Rasimu hii inapaswa kuangalia changamoto za Vijana ili kuzitatua sambamba na kuwasaidia vijana kufika malengo yao”, amesema mmoja wa Vijana, Paul Makoye.
Kwa upande wake kijana Tatu Kassim Sultan, mwenye ulemavu wa Ngozi amependekeza kuwa vijana wa makundi maalum wapewe kipaumbele katika masuala mbalimbali yakiwemo masuala ya Ajira ili kuondokana na vitendo vinavyoashiria unyanyapaa kwa jamii inayowazunguka.
Hii ni mara ya tatu kwa mapitio ya Rasimu ya Sera ya Taifa ya Maendeleo ya Vijana yanafanywa kwa mwaka huu wa 2021 baada ya kwanza kufanyika mwaka 1996 na 2007.
Kundi linahusishwa zaidi
kujadili Rasimu hiyo ni Asasi za Maendeleo za Kiraia, Wawakilishi wa Vijana
kutoka Makundi maalum, Wawakilishi wa Vyama vya Siasa na makundi mengine
Post a Comment