NAIBU WAZIRI BI. MASANJA AFUNGUA KIKAO TFS KUHAMASISHA UTALII.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe.Mary Masanja
akizungumza jijini Dar es Salaam wakati akifungua kikao kazi kilichoandaliwa na
Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) kwa lengo la kuhamasisha Utalii nchini.
NA FRANCISCO PETER.
Wadau mbalimbali nchini wametakiwa kuhamasisha Utalii jambo ambalo litasaidia kuongezeka kwa shughuli za uchumi wa nchini, na uchumi wa mtu mmoja mmoja.
Imeelezwa kuwa sekta ya misitu
mchango wake ni mkubwa tofauti na
inavyoripotiwa kwenye vitabu vya uchumi kuwa ni asilimia 3.5 kwenye pato la
Akizungumza wakati wa akifungua
kikao kazi kilichoandaliwa na Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) kwa lengo
la kuhamasisha Utalii nchini, Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mary Masanja
amesema kuwa Tanzania imejaaliwa neema ya kuwa na uoto wa rasilimali za misitu
kwa asilimia 55 ya eneo la nchi.
Amesema kuwa mchango
wa mistu unaweza kuongezeka kwa kurasimisha shughuli za misitu zitambuliwe kama
vile kukuza viwanda vya kuchakata mazao ya misitu, kurasimisha shughuli za
upandaji miti na ujenzi wa viwanda vya kuchakata mazao ya nyuki.
“Eneo hill lina ukubwa wa wa takribani hekta
milioni 48 ambazo zipo katika maeneo mbalimbali na kusimamiwa na TFS ikiwemo
hifadhi za misitu ya asili, mashamba ya miti, hifadhi za misitu ya mazingira
asili, misitu ya mikoko na misitu iliyo kwenye ardhi ya huria
“Hakuna asiyefahamu
umuhimu wa rasilimali hizi mlizopewa dhamana ya kusimamia, rasilimali
mnazosimamia zina umuhimu mkubwa katika nyanja zote za maisha ya binadamu na
viumbe. Kimazingira rasilimali za misitu zinatunzwa bionuiwai na mifumo
ikolojia inayowezesha uhai wa viumbe vyote,” amesema.
Amesema kuwa bila
misitu hakuna wanyamapori na uhai wa binadamu utakuwa hatarini kwani wote
wanatumia hewa ya oksijeni inayozalishwa na miti na kwamba kijamii misitu yetu
ni muhimu kwa ajili ya shughuli za jadi.
“Hivyo ili
kudumisha utamaduni na mila zetu lazima tutunze misitu yetu ambayo ndio hazina
ya historia yetu,” Amesema.
Amesema misitu ni
muhimu katika shughuli za uchumi wa nchi na uchumi wa mtu mmoja mmoja, na
kwamba mazao mbalimbali yanayozalishwa na msituni kama mbao na magogo
huchakatwa na kuwa bidhaa za viwandani zinazochangia fedha za kigeni na ajira.
Amesema vyanzo
vingi vya maji yanayotumika kwa shughuli za majumbani, mashambani, viwandani na
kwenye mabwawa ya kuzalisha umeme ni misitu.
Shughuli za
uanzishaji misitu binafsi kwa njia ya upandaji miti unawezesha mwananchi mmoja
mmoja kunufaika na fursa za misitu.
Amefafanua bidhaa
za viwandani zinazotokana na mazao ya misitu na ufugaji nyuki zitaongeza
ajira na mauzo ya nje,hivyo kuna jukumu kubwa kuhakikisha rasilimali hizo
zinaendelea kutunzwa na kuendelezwa ili kukidhi majukumu hayo ya kimazingira,
kiuchumi na kijamii kwa kuzingatia kizazi cha sasa na kijacho.
“Serikali meweka
msisitizo mkubwa katika utekelezaji wa majukumu haya. Leo tuko hapa kwa ajili
ya kuzungumzia suala la utalii ikolojia kama zao mojawapo la misitu yetu,
shughuli hii katika dhana ya uhifadhi wa misitu ni mpya na inashamiri kwa
kiwangi kikubwa”.
“Mnafahamu kuwa
wizara imepewa jukumu la kuhakikisha idadi ya watalii inaongezeka kufikia
watalii milioni tano ifikapo mwaka 2025 na kuongeza mapato yanayotokana utalii
kufikia dola za Marekani bilioni sita”. Ameeleza.
Hata hivyo amesema
utalii unachangia zaidi ya asilimia 17 ya Pato la Taifa na asilimia 25 ya
mapato ya fedha za kigeni hivyo mchango huu kwa kiwango kikubwa unachangiwa na
wageni wanaotembelea nchini kwa ajili ya utalii wa wanyama.
“Mchango wa utalii
utaongezeka kama tutahamasisha na kuimarisha utalii ikolojia na kuhamasisha
utalii wa ndani,” amesema na kuongeza anafahamu wizara ilikasimu usimamizi wa
vituo sita vya malikale kwa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania.
Post a Comment