Ads

VIJANA WAMETAKIWA KUTUMIA FURSA KUJIUNGA NA MAFUNZO YA MAPISHI YA KEKI.

 

Mkurugenzi wa Kampuni ya Anezylita Bi. Zena Shariff Scaba akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa duka lake jipya ambalo linajihusisha na masuala ya mapambo ya nyumbani pamoja na shule ya mapishi ya keki.
..................
NA PRANCIS PETER, DAR ES SALAAM.
Wadau wametakiwa kutumia vizuri mitandao ya kijamii kwa kujifunza mambo mbalimbali ambayo yanaweza kuwasaidia katika maisha.

Akizungumza katika uzinduzi wa duka jipya, Mkurugenzi wa Kampuni ya Anezylita Bi. Zena Shariff Scaba, amesema kuwa kampuni hiyo imekuwa inafanya mashindano ya kupika keki ambapo mwaka jana na mwaka huu hayajafanyika kutokana na ugonjwa wa korona, ambapo mashindano hayo yataanza hivi karibuni.
Bi Zena amesema kuwa vijana waliopo nyumbani watapata mafunzo ya mapishi na kupatiwa vyeti vya serikali ya Tanzania hivyo amewataka wachangamkie fursa hiyo.

"Tumeamua kufungua duka jingine ili vijana wajifunze mapishi lakini pia kuuza mapambo ya majumbani kwa gharama nafuu sana, wananchi wajitokeze kutumia fursa hii" amesema Bi Zena.

Amesema kuwa kampuni yake imewezesha kutoa ajira kwa vijana wengi wa kitanzania ikiwa ni sehemu ya kuiunga mkono serikali katika kukabiliana na changamoto ya ukosefu wa ajira.

 Ameiomba jamii itumie vizuri mitandao ya kijamii kujifunza mambo mbalimbali pamoja na kutumia kama njia ya kutangaza biasha za

No comments