Ads

FISH4ACP NA TAFIRI KUINUA MNYORORO WA THAMANI UVUVI WENYE TIJA ZIWA TANGANYIKA.

Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Utafiti wa Uvuvi nchini (TAFIRI) Dkt. Ismael Kimirei akizungumza na waandishi wa habari leo Mkoani Kigoma nje ya mkutano wa FISH4ACP uliofanyika ukumbi wa mikutano wa NSSF kuhusu na Uvuvi wenye tija Ziwa Tanganyika.

 

Wavuvi wadogo pamoja na wafanya biashara wa rejareja na wachakataji wa samaki Mialo ya Ziwa Tanganyika, Kigoma wakishiriki katika kuchangia mawazo kuhusu mradi wa FISH4ACP

Na Francisco Peter, Kigoma.

Taasisi ya Utafiti wa Uvuvi nchini (TAFIRI) kupitia mradi wa FISH4ACP unafadhiliwa na Umoja wa Ulaya (EU) na Serikali ya Ujerumani wameandaa warsha Mkoani Kigoma ambapo imewakutanisha wadau mbalimbali wakiwemo wafanyabiashara wadogo katika ziwa Tanganyika kwa ajili ya utatekelezwa mradi wa kuwasaidia wavuvi katika nchi 12 ikiwemo Tanzania.

Katika mradi huo Tanzania imenufaika kwa kutengewa kiasi cha euro milioni tatu, ambapo umelenga kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili wavuvi, wasafirishaji wa samaki aina ya migebuka, dagaa wa Kigoma na masoko ya ndani na nje ya nchi katika ziwa Tanganyika.

Akizungumza leo Mkoani Kigoma katika warsha  ya wadau mbalimbali ilioandaliwa mradi wa na FISH4ACP, Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Utafiti wa Uvuvi nchini (TAFIRI) Dkt. Ismael Kimirei, amesema kuwa wanaangalia changamoto  mbalimbali zinazowakabili wavuvi, wasafirishaji wa samaki aina ya migebuka, dagaa wa Kigoma na masoko ya ndani na nje ya nchi katika ziwa Tanganyika.

Dkt. Kimirei amesema kuwa kupitia mradi wa FISH4ACP ambao utatekelezwa kwenye nchi 12 ambao unafadhiliwa na umoja wa ulaya (EU) na serikali ya ujerumani unagharimu kiasi cha Euro Milioni 40, huku Tanzania ikinufaika na mradi huo kwa kutengewa kiasi cha euro milioni tatu.

"Ingawa myororo wa uchumi kwa ujumla unalipa kwa watendaji wa mnyoro huo kwa baina ya asilimia 12 na 45 kuna mwenendo wa kushuka kwa mapato kadri usambazaji wa samaki ulivyopungua baada ya muda" amesema Dkt. Ismael.

Amesema kuwa matumaini yake kuwe na wadau mbalimbali katika warsha hiyo ili waweze kuchangia mjadala mpana na wenye tija katika kuboresha mnyororo wa thamani wa dagaa migebuka wa Ziwa Tanganyika.

Mwakilishi wa Shirika la Chakula na Kilimo Duniani (FAO) Bw. Adam Sandall akishiriki warsha hiyo kwa njia ya mtandao kutoka  London Uingereza, amesema kuwa asilimia 6% tu ya migebuka ndiyo inayosafirishwa kwenda nchi za nje.

Mfanyabiashara mdogo katika ziwa Tanganyika Bi. Suzan Ezekiel katika mwalo wa kibirigi Ujiji, amesema kuwa ujio wa mradi wa FISH4ACP ni njia sahihi katika kuwakwamua kiuchumi.

No comments