TMDA YAANZA RASMI KUTOA ELIMU KUHUSU MATUMIZI YA BIDHAA ZA TUMBAKU.
Mkurugenzi mkuu wa Mamlaka ya dawa na vifaa tiba (TMDA) Bwana Adam Fimbo, wapili kutoka kulia akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya watumishi wa Mamlaka ya dawa na vifaa tiba (TMDA)
Mamlaka ya dawa na vifaa tiba (TMDA) imesema imeanza kuweka utaratibu na mfumo katika kudhibiti wa bidhaa za tumbaku.
Hayo yamebainishwa na mkurugenzi mkuu wa malaka hiyo Bwana Adam Fimbo, katika viwanja vya maonesho ya biashara ya kimataifa (Sabasaba ) wakati akizungumza na waandishi wa habari katika banda la mamlaka hiyo.
"Kuanzia mwezi wanne mwaka huu tumepewa kazi ya kudhibiti bidhaa za tumbaku na waziri wa Afya ,sheria ilikuwepo tangu mwaka 2003 lakini hapakuwepo na malaka rasmi ambayo iliundwa kwaajili ya kusimamia na kudhibiti bidahaa hiyo" Amesema
Amesema kupitia sheria hiyo TMDA imejikita zaidi katika kutoa elimu kwa wananchi kuhusu madhara ya tumbaku ambayo ni magonjwa yasiyo ya kuambukiza kama Kansa za koo,mapafu , shinikizo la damu magonjwa kwenye mfumo mzima wa Moyo na damu .
Sheria hii pia inazuia watu wenye chini ya umri wa miaka 18 kuvuta sigara ,na pia tumbaku ambazo hazivutwi haziruhusiwi kutumika.
"Tutaendelea kuwapa elimu wale wote wananotumia tumbako na kuvuta sigara ili waache taratibu nawale ambao hawajajiingiza katika matumizi ya tumbaku waache kabisa kutokana na madhara haya niliyo yaeleza nikazi kubwa lakini tumejipanga kuitekeleza kama tunavyo fanya katika dawa, vifaa tiba na vitendanishi"Amesema.
Sheria hii pia inaeleza kuhusu kutenga maeneo maalumu ya kuvuta sigara hasa maeneo yanayo husisha watu wengi ili moshi usiwafikie watu wengine ambao hawavuti.
"Meneo ya migahawa,baa na mikusanyiko mbalimbali inayoleta watu karibu inapaswa kuwa na maeno hayo ,mtu ambaye havuti sigara anapo puliziwa moshi na mvutaji anapatwa na madhara haya"Amesema.
Kwa maelzeo zaidi fika katika banda la TMDA katika viwanja vya maonesho ukumbi wa Kilinjaro ili kupata elimu zaidi
Post a Comment