Idadi ya wawekezaji yaongezeka ,TIC wafunguka mazito sabasaba.
Kituocha uwekezaji Tanzania (TIC) kimesema kuanzia miezi mitatu iliyopita idadi ya wewekezaji waliosajilwa na kituo hicho imeongezeka kwa kulinganisha na wakati uliopita.
Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi mtendaji wa kituohicho Bwana Maduhu Kazi wakati akizungumza na waandishi wa habari katika banda la kituo hicho lililpo ukumbi wa Karume.
Amesema kwa mara ya kwanza mwaka huu wa fedha uwekezaji umepanda kwa kipindi kifupi ambapo miradi zaidi ya 235 ukilinganisha na miradi 2019 iliyo sajiliwa mwaka wa fedha uliopita.
"Tumeweza kukuza ajira kwa miradi hii iliyosajiliwa na tutaweza kupata miradi mingi zaidi na sasa tumeanza kutoa maeneo ya kujenga Indastrial Parks na pia tuna wawekezaji wanne tuko nao katika mazungumzo wameonesha nia ya kujenga Indastria Parks''Amesema
Aidha amesema ameelezakuwa sheria ya uwekezaji haina ubaguzi kwa wawekezaji iwe wa nadani au wa nje bali imetoa unafuu kwa wawekezaji wazawa mfano Wawekezaji wa ndani husajiliwa kuanzia na mtaji wa Dolla 100,000.00 /= kwenye mradi na wale wawekezaji wa nje husajiliwa kuanzia Mtaji wa Dolla 500,000.00/= .
Kituo cha uwekezaji Tanzania (TIC) kinawakaribisha wananchi wote wanaotembelea maonesho ya 45 ya biashara ya kimataifa yanayo fanyika katika viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere (Sabasaba) Kilwa road jijini Dar es salaam, kutembelea banda lake ili waweze kujifunza mambo mbalimbali ikiwemo huduma zinazo tolewa .
Post a Comment