Mkurugezi PBZ, huduma za bank ya watu wa zanzibar ni nafuu sana ,soma hapa kujua
Banda la Bank ya watu wa Zanzibar PBZ lipo katika ukumbi wa Karume
Bank ya watu wa Zanzibar PBZ imesema sababu ya watu wengi kuipenda Bank hiyo ni kutokana na huduma nzuri zinazotolewa ikiwemo mikopo nafuu kwa wafanyakazi .
Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi mwendeshaji wa Bank ya watu wa Zanzibar PBZ , Dakta Muhsin Salim Masoud wakati akizungumza na waandishi wa habari katika maonesho ya 45 ya biashara ya kimataifa yanayofanyika katika viwanja vya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.
Amesema Maonesho hayo yamesaidia Bank hiyo kujitangaza huduma zake kwa wananchi wanaotembelea banda lao na watu wengi wameweza kufungua Account ,na kupata kadi za VISA kwa haraka.
"Muonekano wa Bank ya PBZ zamani ilikuwa inaonekana kama Bank ya Zanzibar Pekee wala siyo ya Tanzania Bara lakini hapa tumepata nafasi ya kuwa eleza kuwa Bank hii ni ya watu wote na imeenea sana Zanzibar na hapa bara "Alisema
kumoja ya mafanikio yake makubwa n 'inawakaribimeishauri mamlaka ya maendeleo ya biashara Tanzania
Bank hii makao makuu yake yako Zanzibar inayo matawi sehemu mbalimbali matawi 16 bara na Zanzibar tuna huduma za usafirishaji fedha nje ambazo ni zaharaka na kuaminika ,tunatoa mikopo nafuu kwa wafanyakazi wa serikali "Amesema
Pia amesema Bank hiyo inampango wa kufungua matawi maeneo mbali mbali ikiwemo Tazara ,Lumumba ,kigamboni ,Tandika ,Arusha na Mwanza, Mtwara na karibuni litafunguliwa tawi jipya Tandahimba .
Aidha Dakta Muhsin amesema, Bank hiyo ina kitengo maalumu cha Bank ya kiislamu ambacho kinafanya miamala yake kwa kufuata sharia za kiislamu.
"Tofauti ya Bank hii na Bank nyingine ni kwamba yenyewe haiuzi pesa kwa pesa ila ukitaka kuwezeshwa unawezeshwa kupitia vitu ,kwahiyo Bank inafanya biashara na wewe inachukua risk siyo ile bank ambayo inaacha risk zote kwa mteja "Amesema.
Post a Comment