Ads

PROF.SHEMDOE ATOA SIKU 45 UJENZI WA CHOO CHA SHULE YA MSINGI

 



Na Mwandishi wetu – Kilimanjaro

Serikali imeelekeza kiasi cha fedha shilingi Mil.8, zilizochangwa na wananchi, fedha za ushirika pamoja na zilizovuka mwaka zitumike kuimarisha Miundombinu ya Shule ikiwepo Choo cha Shule ya Msingi Umbwe, iliyopo mkoani Kilimanjaro.

Akiwa katika Ziara ya kikazi kukagua, shughuli za maendeleo, Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais -Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Prof. Riziki Shemdoe, alisema ametoa kipindi cha siku 45 kwa uongozi wa Shule hiyo, kuhakikisha wanatumia kiasi cha shilingi Mil.8 zilizochangwa na wananchi na zile za Chama cha Ushirika kukamilisha ujenzi wa Choo na kutaka kupelekewa taarifa ifikapo tarehe 30. Agosti, 2021.

“Fedha za mapato ya ndani ambazo zimevuka mwaka kupitia mfumo wa MUSE, pindi mfumo ukifunguliwa, zipelekwe mara moja kwa ajili yakukamilisha Miundombinu ikiwepo Choo cha Shule hii” ameelekeza Shemdoe.

Katika hatua nyingine, Prof. Shemdoe, akiwa katika Shule ya Sekondari ya Umbwe, ameelekeza kuongezwa kwa wanafunzi 32 wakati wa zoezi la chagua la pili la wanafunzi wanaojiunga kidato cha Tano ili Shule hiyo iweze kuchukua wanafunzi 700 ambao ndio uwezo wa Shule tofauti na sasa ambapo Shule hiyo ilipelekewa wanafunzi 668 tu.

“Pamoja na kuongeza idadi ya wanafunzi hao 38 lakini pia ameagiza atafutwe Mwalimu mmoja wa Masomo ya Uchumi, Komasi na Mahesabu (ECA), ili waweze kuwa na msawazo wa Mwalimu mmoja kwa wanafunzi 30” amesisitiza Shemdoe.

Akiwa katika ziara hiyo, Prof. Shemdoe alitumia fursa hiyo kuelekeza kiasi cha fedha shilingi Mil.150 zitumike kukarabati jengo la Utawala na Nyumba za Mwalimu.

Mbali na maelekezo hayo ya ujenzi na Ukarabati wa Miundombinu, Prof. Shemdoe, ameuagiza Uongozi wa Elimu katika Halmashauri ya ya Wilaya ya Moshi, kuona namna nzuri yakuunganisha baadhi ya Shule zenye wanafunzi wachache ili rasilimali zilizopo zeweze kutumika vizuri.

“Hapa kwenu kuna Shule za Msingi zina wanafunzi wanaozidi 70, angalieni uwezekano hasa kwa shule zile zilizopo jirani, mziunganishe, lakini zingatieni umbali kati ya mwendo wa mwanafunzi na shule ilipo”.

Wakati huo huo, Katibu Mkuu, Shemdoe ameutaka uongozi wa TARURA wilayani humo, wabunge na Madiwani katika Jimbo hilo kukaa kwa pamoja na kujadiliana juu ya matumizi ya fedha shilingi Bil. 1.5 zitumike vipi katika Jimbo hilo.

Prof. Shemdoe yupo mkoani humo kwa ziara ya kikazi ikiwa ni muendelezo wa ukaguzi wa shughuli za maendeleo.

No comments