Ads

Mbunge wa Manyoni Magharibi akutana na wananchi kijijini Damwelu soma mipango walijadili

 

Mbunge wa Manyoni Magharibi Yahaya Omary Massare amesema kuwa atachangia ujenzi wa Zahanati  kwa  wananchi wa Kijiji cha Damwelu kata ya Ipande wilaya ya manyoni Mkoani Singida endapo wananchi wa kijiji hicho watajitolea  kuanzisha ujenzi  huo.  

            Hayo yamesemwa na Mbunge huyo alipokuwa akizungumza na wanakijiji wa kijiji hicho kwenye mkutano wa hadhara ulioandaliwa na Mbunge huyo wenye nia ya kuwashukuru kwa kumpigia kura za kutosha  pamoja na kueleza mikakati iliyopo na iliyotekelezwa tangu alipochaguliwa  mwaka 2020.                                    

Aidha amewataka wanakijiji hao kushirikiana na uongozi wa kijiji katika masuala mbalimbali ya maendeleo ikiwemo kuboresha miundombinu mbalimbali na huduma za kijamii.     

        Akijibu kero ya umeme iliyoelezwa na Diwani wa kata ya Ipande Kedmon Japhet Mpondo amesema kuwa tayari amepokea fedha kwa ajili ya usambazaji umeme katika vijiji 15 na tayari Mkadharasi amepatikana na atatangazwa wiki ijayo na kuanza kazi rasmi.    

                               Massare pia amewataka viongozi wa vijiji kushirikiana na wakala wa umeme vijijini REA watakapofika kuwainyesha maeneo ya makazi wa watu kwa ajili ya kuweka nguzo ili kuhakikisha kuwa wananchi wa vijiji hivyo wanapata umeme pasipokuwa na bughudha yoyote.       

                        Aidha amewataka viongozi wa dini zote kushirikiana na viongozi wa kijiji cha Damwelu kuhakikisha kuwa wanatoa elimu ya kutosha kwa wananchi ilinkujitokeza kwa wingi katika kushiriki zoezi la sensa mwaka 2022.     

         Naye Diwani wa kata hiyo  Kedmon Japhet Mpondo amemuomba mbunge huyo kuzidi kywasaidia katika kuboresha elimu katika kata hiyo jambo ambalo limejibiwa na Mbunge kuwa lengo ninkuhakikisha kuwa kijiji cha Damwelu kinakuwa na shule Mbili za Msingi  ikiwemo kurasimishwa shule ya msingi Mgamboo kuwa shule kamili.      

           Mkutano huo ulihudhuriwa na wananchi wa kijiji cha Damwelu na viongozi mbalimbali wa vyama na serikali kutoka katika kijiji na kata ya Ipande.

No comments