Pact Tanzania Yataja Kutoa Jumla ya Ajira 9,595 kwa Vijana
Shirika Pact Tanzania imefanikiwa wamepatiwa ufadhili wa mafunzo ya ufundi stadi na zana za kujiongezea kipato vijana takribani 9,595 kuanzia mwaka 2018 hadi hivi sasa nchi Tanzania na vile vile imekuwa likifanya juudi kwa kushirikiana na wadau wa sekta binafsi katika maendeleo ya jamii.
Ufadhili huo umetolewa na Shirika hilo lisilo la kiserika linalofanya kazi katika nchi zaidi ya 35 duniani ambapo kwa nchini likiwa limetimiza miaka 50 ,kupitia utekelezaji wake wa miradi ya USAID Kizazi kipya pamoja na ACHIEVE limetaja kuwa hali hiyo imekuja kupitia ufadhili wa Mfuko wa Dharura wa Rais wa Marekani wa Kupambana na UKIMWI kupitia Shirika hilo la Marekani la Maendeleo ya Kimataifa USAID.
Akizungumza jijini Dar es Salaam Mkurugenzi Mkazi (USAID) Mariana Balampama ameiomba TAMISEMI wawapigie chapuo vijana hao iliwapate kandarasi kupitia miradi mbalimbali mbali inayotekelezwa katika halmashauri zote kwa kuwa tayari wapo vijana walioweza kupata mafunzo katika fani za ufundi magari, ushonaji , upambaji na fani zingine.
"Kati yao vijana 605 watapata zana hizo mwaka huu , wahenga walisema " hakupaye samaki anakusitiri kwa chungu kimoja ; akupaye nyavu anakustihi milele,"amesema Marianna.
Aliongeza kuwa ni furaha yao kuwa vijana hao hawaondoki hapo na samaki , wanaondoka na nyavu , wanaondoka na manoari ili waende wakavue bahari ya mbali .
Wakati huo huo Francis Pirimin Komba ambaye ni mratibu wa mafunzo ya uanagenzi pacha aliye mwakilisha Mkurugenzi Mkuu wa (VETA) Dkt.Pancras Bunjulu amesema kwa sasa wanavyuo zaidi ya 40 Tanzania na kuwa vijana wote wakijengewa stadi ya maisha mambo yataenda vizuri.
"Sehemu ya kujifunza ujuzi ni sehemu nzuri katika maono ya maendeleo ya vijana sisi tunatoa ujuzi katika fani zaidi ya 90 hivyo wajitokeze ambapo kwa sasa kuna vyuo 25 vinakwenda kujengwa vijijini," amesema Komba.
Katika hatua ya kuimarisha mifumo ya utoaji huduma kwa watoto walio katika mazingira hatarishi ; mradi wa ACHIVE umetoa viti 156, makabati ya chuma 1033 pamoja na zana mbali mbali za kukusanyia taarifa.
Shirika hilo jana pia waliweza kufanya makabidhiso hayo y.a vifaa ambapo walialika Wilaya ya Ilala kuwawakilisha maeneo ya halmashauri zingine nchini juu ya makabidhiano hayo.
Mkuu wa Wilaya ya Ilala Dar es Salaam Ng'wilabazu Lugigija amelipongeza Shirika hilo lisilo la kiserika .
"Napongeza harakati katika mikakati yao kwani wamekuwa kichocheo kukuza uchumi kwa kuzingatia maendeleo ," amesema Ludigija
Post a Comment