Kituo cha uwekezaji Tanzania (TIC) chatoa fursa kwa wananchi sabasaba.
Afisa habari na uhusiano wa kituo cha uwekezaji Tanzania (TIC) Bi Robertha Makinda , akizungumza na wateja waliotembelea banda hilo katika maonesho ya 45 ya biashara ya kimataifa katika viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere (Sabasaba) Kilwa road jijini Dar es salaam.
Kituo cha uwekezaji Tanzania (TIC) kinawakaribisha wananchi wote wanaotembelea maonesho ya 45 ya biashara ya kimataifa yanayo fanyika katika viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere (Sabasaba) Kilwa road jijini Dar es salaam, kutembelea banda lake ili waweze kujifunza mambo mbalimbali ikiwemo huduma zinazo tolewa .
Akizungumza na Waandishi wa habari , Meneja uhamasishaji uwekezaji Kanda ya Nyanda za juu kusini wa kituo hicho Bwana, Venance Mashiba, amesesema kituo cha uwekezaji Tanzania kinashiriki maonesho hayo kwa lengo la kuufahamisha umma kuhusu shughuli za taasisi hiyo ambayo iko chini ya Serikali.
Amesema moja ya majukumu ya kituo hicho ni kuhamasisha wawekezaji ,kuwasajili wawekezaji walio itikia wito wa kuwekeza ,katika makundi yote mawili wawekezaji wa ndani na wanje.
Wawekezaji wa ndani husajiliwa kuanzia na mtaji wa Dolla 100,000.00 /= kwenye mradi na wale wawekezaji wa nje husajiliwa kuanzia Mtaji wa Dolla 500,000.00/= na baadaye huanza kuwa hudumia kupata kibali na ardhi ya uwekezaji.
AIdha ameeleza kuwa, kituo hicho pia huwahudumia wajasiliamali wadogo kwa kuwajengea uwezo , kuwapatia mafunzo na kuwa unganisha na wewekezaji wakubwa .
Amesema Tanzania inazo fursa nyingi za uwekezaji na ili kujifunza zaidi wananchi wanashauriwa kutembelea banda la TIC , lililopo banda la Karume stand namba moja.
Post a Comment