Ads

Soma hapa kujua timu ya Simba ilivyo endeleza uteja kwa Yanga

 

Klabu ya Yanga   imeendeleza ubabe  kwa watani wao Simba  baada ya pata ushindi wa bao 1-0  katika mchezo uliopigwa kwenye dimba la Benjamin Mkapa ukishududiwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan .


Bao pekee la Yanga SC lilifungwa na Kiungo wa Klabu hiyo, Zawadi Mauya dakika ya 11 ya mchezo baada ya kupiga shuti kali lililomgonga Beki wa Simba SC, Shomari Kapombe na kutinga wavuni likiwaacha Simba wakishangaa dakika za mwazo za mchezo huo.


Yanga SC walionekana kumudu mchezo huo na kucheza kwa kujiamini na ufundi wa hali yajuu  dakika zote ingawa wapinzani wao walionekana kuzinduka dakika za mwisho wakijaribu kulisakama lango la Yanga  bila mafanikio 


Mabeki wa pembeni wa Yanga SC, Kibwana Shomari na Adeyum Salehe walionekana kumbana vilivyo Mchezaji  wa Simba SC, Bernard Morrison na kukosa nafasi ya kufurukuta pamoja  na kubadilishwa nafasi za kuza mara tatu,   safu ya Kiungo kikiongozwa na Clatous Chama nayo haikufua dafu.

Simba SC  ambayo sasa  ambapo ni moja ya timu zinazo endeleza uteja kwa Yanga , imeshindwa kutangaza Ubingwa wa Ligi Kuu Bara (VPL) mbele ya Yanga SC ,sasa itasubiri michezo yake iliyobaki katika Ligi hiyo dhidi ya Azam FC, Namungo FC, Coastal Union na KMC FC.

Watani hao wa jadi kwa mwaka huu mpaka sasa wamekutana mara mbili ambapo mwanzoni january mwaka huu walikutana katika kombe la mapinduzi zanzibar ambapo Yanga pia ilishinda na kutwaa kombe.

No comments