IGP SIRRO ALAANI VITENDO VYA MAUAJI
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro amesema kamwe vyombo vya ulinzi na usalama likiwemo Jeshi la Polisi havitatoa mwanya kwa makundi ya watu au mtu kuweza kuvuruga hali ya amani na usalama sambamba na kutekeleza vitendo vya kihalifu na mauaji.
IGP Sirro amesema hayo leo Moshi mkoani Kilimanjaro wakati akizungumza na Wenyeviti wa serikali za mitaa, Watendaji Kata pamoja na viongozi wa vikundi vya ulinzi shirikishi ambapo amewataka kutambua wajibu wao na kuchukua hatua kwa wanaovunja sheria.
Naye Mwenyekiti wa Kamati ya Amani Mkoa wa Kilimanjaro Askofu Jones Mola, ameihasa jamii kuendelea kushirikiana na Jeshi la Polisi kwa kutoa taarifa sahihi za uhalifu hatua ambayo itawezesha kukamatwa kwa wanaojihusisha na vitendo hivyo.
Post a Comment