TBS YATOA MUONGOZO TAASISI KUTUMIA MAABARA ZILIZOPATA CHETI CHA ITHIBATI YA UMAHIRI
Afisa Udhibiti
Ubora wa TBS, Bi.Stella Mrosso akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi
za TBS leo Jijini Dar es Salaam.
NA NOEL RUKANUGA, DAR ES SALAAM
Shirika la Viwango Tanzania (TBS) limewaasa Taasisi za serikali
au binafsi kutumia huduma za maabara zilizopata cheti cha ithibati ya Umahiri.
Ameyasema hayo leo Afisa Udhibiti Ubora wa TBS, Bi.Stella Mrosso
akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi za TBS Jijini Dar es Salaam.
Amesema Tanzania kuna maabara arobaini na mbili (42) ambazo
zimepata ithibati ya umahiri kutoka SADCAS, ambazo ni maabara za hospital, za
upimaji wa vyakula, upimaji maji, chemikali, mafuta ya magari, vifaa vya ujezi,
umeme, uhandisi mitambo na maabara za kupima madini.
Aidha Bi.Stella amesema kuwa kwa kutumia huduma zenye Ithibati
tutaweza kutekeleza Malengo ya Maendeleo Endelevu ya Umoja wa Mataifa (UN SDGs
2030).
“Ithibati ya umahiri inaweza kutolewa kwa taasisi zinazotoa
huduma ya upimaji,(mfano maabara za hospital, maabara za kwenye taasisi za
uthibiti ubora, vyuo vya elimu na tafiti, taasisi za kilimo na mifungo)
ugezi, ukaguzi na uthibitishaji wa bidhaa na huduma mbalimbali ili
kujenga imani kwa watumiaji kuwa bidhaa na huduma inafaa kwa watumizi
yaliyokusudiwa”. Amesema Bi.Stella.
Pamoja na hayo amesema taasisi zenye Ithibati ya umahiri ni
kielelezo kwamba zimetengeneza na zinatekeleza mifumo ya viwango vya kimataifa
(international standards) wakati wa kutekeleza majukumu yake ya kimsingi ili
kufikia lengo lililokusudiwa.
Hata hivyo amesema kuwa Viwango vya kimataifa vinavyohusu
maswala ya ithibati ni Pamoja na ISO 17025 Matakwa ya umahiri kwa ajili ya
maabara za upimaji na ugezi, ISO 15189 Matakwa ya umahiri kwa ajili ya maabara
za hospitali, ISO 17020 Matakwa ya umahiri kwa ajili ya ukaguzi, ISO 17065
Matakwa ya umahiri kwa ajili ya uthibitishaji wa bidhaa, ISO 17021 matakwa kwa
taasisi zinazofanya kaguzi ya mifumo ya ubora (certification bodies that
conduct managements systems audits).
Amesema faida ya ithibati ni pamoja na kupunguza gharama za
kufanya biashara (tested once accepted every where), inasaidia kuondoa vikwazo
vya biashara, Kuboresha utendaji kwa kutambua vihatarishi na kuviwekea mkakati
wa kuvizuia, Kuwezesha utendaji wenye tija na endelevu na pia Inasaidia
technology transfer.
Post a Comment