BUNGE LAMTHIBITISHA ZUNGU TENA
Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limewathibitisha Mbunge wa Ilala, Mussa Azzan Zungu, Mbunge wa Viti Maalum, Najma Giga na Mbunge wa Mufindi Kusini David Mwakiposa kuwa Wenyeviti wa Bunge.
Bunge limewapitisha wabunge watatu kuwa wenyeviti wa chombo hicho cha kutunga sheria watakaokuwa wasaidizi wa Spika na naibu wake.
Naibu Spika wa Bunge, Dk Tulia Ackson amewaomba wabunge kuridhia majina hayo baada ya kupitishwa na kamati ya uongozi wa Bunge.
Baada kuwahoji wabunge, wote waliitikia kwa sauti za ndiyo na hakukuwa na kura iliyowakataa huku watatu hao wakiahidi kufanya kazi kwa weledi.
Post a Comment