WADAU WA BIASHARA NA WAMILIKI WA VIWANDA WATAKIWA KUITUMIA ELIMU INAYOTOLEWA NA BRELA
Ofisa Leseni Rajab Chambega akitoa elimu kuhusu namna ya upataji wa leseni za viwanda na biashara katika semina kwa wajasiliamali na wafanya biashara iliyofanyika katika ukumbi wa SIDO mkoani Njombe.
Na Christina Njovu-Njombe
WADAU wa bishara na wamiliki wa viwanda vidogovidogo mkoani Njombe wametakiwa kutumia elimu inayotolewa na Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) na kuwaelimisha wengine ili waweze kurasimisha biashara zao ili ziweze kutambulika kisheria.
Akizungumza wakati wa warsha ya utoaji elimu ana kwa ana kuhusu huduma zinazotolewa na BRELA iliyofanyika katika ukumbi wa SIDO mkoani Njombe Mwenyekiti wa TCCIA Mkoa wa Njombe Menerad Mlyuka amesema elimu hiyo inayotolewa na BRELA ni muhimu na kila mmoja ni vema akasikiliza kwa makini na kuielewa.
"Kila mmoja asikilize na apate ufahamu ili akaweze kuitumia hii elimu vizuri zaidi na akawafundishe na wengine , kwa kutumia pia vyombo vya habari vilivyoshiriki natumaini elimu hii itaweza kuenea katika mkoa mzima wa Njombe,"amesema Mlyuka.
Wakitoa pongezi kwa BRELA kwa kuamua kutoka na kuwapatia elimu hiyo mmoja wa washiriki hao bibi Roida Emanuel Mng'ong'o ambaye ni mjasiriamali wa usindikaji wa asali na pia ni muuzaji wa asali alieleza kuwa aliwahi kupata elimu kuhusu BRELA kutoka kwa watu ambao sio sahihi kiasi ambacho alishindwa kuelewa nini afanye katika kuendelea kuhuisha biashara yake.
Kutokana na elimu hii iliyotolewa na BRELA mkoani Njombe imemuwezesha kuifahamu vizuri BRELA ikiwa ni pamoja na kutambua kuwa anatakiwa kuhuisha biashata yake kila mwaka ili iweze kutambulika ndani ya nchi hata nje ya nchi.
Aidha washiriki hao walitoa mapendekezo yao ya kutaka taasisi nyingine zinazotoa huduma kama BRELA kushirikiana kwapamoja katika kutoa elimu ili wadau waweze kutambua mipaka na majukumu ya kila taasisi ambazo walizitaja baadhi kuwa ni pamoja na TBS na TRA na TFDA.
Wameongeza kuwa BRELA inatakiwa kutoka ofisini na kufika hadi katika wilaya ili wafanyabishara na wadau wa biashara waweze kupata huduma stahiki kwa usahihi kutoka kwa wahusika wakuu tofauti na ilivyo sasa ambapo baadhi ya wale wanaojiita BRELA wanashindwa kuwahudumia ipasavyo badala ya mteja kuondoka akiwa ameridhika badala yake anaondoka akiwa na sononeko.
BRELA ipo katika kazi ya kutoa elimu kwa umma mkoani njombe ambapo pamoja na kukutana na wadau ana kwa ana pia imetoa elimu hiyo kwa njia ya redio za kijamii ili wananchi hadi walio vijijini waweze kuelewa namna ya urasimishaji biashara zao kwa kusajili majina na alama za biashara zao na kuacha kutumia vyeti vya watu wengine katika kutoa huduma ama kufanya biashara.
Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni inafanya kazi zake kwa mjia ya mtandao, ambapo mtu yeyote anayehitaji kufanya sajili atapata hiyo huduma kwa njia ya mtandao, ikiwa atakumbana na changamoto atatakiwa kupiga namba +255 (0)222 212 800 ambapo ataweza kupata maelekezo zaidi.
Baadhi ya washriki wakifuatilia Semina ya utoaji elimu juu ya namna ya upataji wa huduma zitolewazo na BRELA zikiwemo upataji leseni za viwanda na biashara katika semina kwa wajasiliamali na wafanya biashara iliyofanyika katika ukumbi wa SIDO mkoani Njombe.
Wafanyakazi wa BRELA wakitia elimu kwa umma juu ya huduma zinazitolewa na Wakala katika kituo cha redio Uplands kilichopo Mkoani Njombe.
Post a Comment