Ads

Wadau madinini ya Copper walia na changamoto zinazozorotesha huduma

WADAU wa Madini Tunduru wilayani Songea Mkoani Ruvuma walia kukosa utetezi wa usimamiaji shughuli za madini hali inayopelekea kuibuka kwa changamoto mbalimbali zinazozorotesha huduma pamoja na Serikali kukosa takwimu halisi za upatikanaji wa madini katika eneo husika.

Amesema wanapambana kuhakikisha ujenzi wa kiwanda kitakachokuwa kikiyapandisha thamani madini ya Copper kikikamilika kwa kutoa ajira kwa watu 300 ambacho kitakuwa na uwezo wa kuingiza kwenye mtambo karibu tani zipatazo 500.

Akizungumza na vyombo vya habari jijini Dar es Salaam Mchimbaji mdogo wa madini ya Copper Benson Mwakilembe alisema kwa nyakati tofauti wachimbaji wadogo wa madini wamekuwa na changamoto  za ukosefu wa zana bora za kufanyia kazi na mikopo hali inayopelekea shughuli zao kukwama.

"Kutokana na changamoto mbalimbali zinazotukabili wachambaji wadogo katika migodi yetu ya madini ya Copper ambayo hutoa asilimia 10,15,20 hadi 40 tulihitaji wawekezaji ambao watakuwa na uwezo wa kuwekeza hatua hiyo ilikuja baada ya maelekezo ya Serikali kusimamisha shughuli za usafishaji mizigo kwenda nje," alisema Mwakilembe

Aidha Mwakilembe alidai uwepo wa mizigo katika migodi yao ambayo inasubiri nguvu kazi ya kutosha ambapo ukosefu mitaji ya kutosha na zana hafifu za kutomudu ufanyaji wa shughuli hiyo zimepelekea kudidimia kwa huduma za uchimbaji madini katika maeneo hayo.

Hata hivyo nchi hii imekuwa kinara katika kuongezeka kwa madini ya dhahabu,Tanzanite na Copper lakini yamekuwa yakionekana katika mitandao tu pasipo wenye dhamana kufatilia ama kuifahamisha serikali dhidi ya upatikanaji wa madini hayo.

Alieleza kuwa ili nchi yetu iweze kuinuka kiuchumi inatakiwa kuwepo na uangalizi wa karibu kutoka kwa viongozi kwenye migodi watakaosimamia masuala ya madini kwa kubainisha changamoto zinazowakabili wachimbaji hao kwa kuwapa mbinu wezeshi zitakazowasaidia kufikia malengo.

Kwa niaba ya wachimbaji wadogo ameishukuru Serikali ya Dkt.John Pombe Magufuli kwa kuwafungulia milango ya kuwapunguzia tozo mbalimbali wadau hao na baadhi ya sheria zilizokuwa mwiba katika tasnia ya uchimbaji wa madini hapa nchini.

Pia amemshukuru Waziri wa madini Mh.Dotto Biteko ambapo ameeleza kuwa ameonesha juhudi kubwa na nia ya kuwaonesha njia wadau hao katika kufikia malengo ya mafanikio.

No comments