Ads

Wenye uhitaji wapewa msaada Ocean Road

Katika kuadhimisha siku 16 za kupunguza ukatili wa kijinsia Mtandao wa Polisi Wanawake umetoa msaada kwa wagonjwa na wenye uhitaji katika taasisi ya saratani ya Ocean Road .

Akitoa msaada huo jana Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Mtandao wa Polisi Viwanja vya Ndege Johari Said alisema msaada unajumuisha vifaa ikiwemo kandambili,Maziwa , Sabuni za kuogea , Maji ya Kunywa pamoja na vifaa vingine vya wanawake .

Alibainisha msaada umelenga muendelezo kupinga ukatili huo na kuwa msaada huo umetolewa na vikosi viwili  vya Polisi Anga na kwamba jamii inakumbushwa kupinga ukatili huo kwa wanawake na watoto hivyo kwa pamoja .

" Tumekuja hapa kutoa sapoti kwa wanawake watoto wagonjwa wenye uhitaji kuendeleza kupinga vitendo vya ukatili dhidi yao,"alisema Johari.

Kwa upande wake mwenyekiti wa mtandao huo kutoka Polisi Anga Flora Focus alisema wametoa msaada wa kuendeleza kuadhimisha siku hizo na kwamba umelenga kuwasaidia wanawake na wenye na wenye uhitaji na wasioweza kukidhi kupata .

Akipokea msaada huo mwakilushi wa taasisi hiyo Jesca Lugwene alishukuru mtandao huo na kwamba watautumia katika makundi hayo na kuomba taasisi zingine kuiga mfano wa wanawake hao.

Pichani ni Mtandao wa Polisi Wanawake Dar es Salaam uliofika kutoa msaada kwa wagonjwa na wenye uhitaji katika taasisi ya Saratani ya Ocean Road jijini humo jana.

No comments