DC KIGAMBONI ATOA SOMO KUHUSU MAJI YA DAWASA.
Na John Luhende
Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Mhe. Sarah Msafiri amewataka wakazi wa kata ya Kigamboni kuyaamini maji ya DAWASA kwani ni majisafi na salama.
DC Msafiri ameyasema hayo leo akiwakatika mkutano wa hadhara uliowakutanisha wananchi na DAWASA kujadili kero za maji zinazo wakabili baada ya mamlaka ya maji kuanza kutoa huduma za maji katika kata hiyo ambapo awali wananchi walikuwa wanatumia maji ya visima ambayo usalama wake si wakuaminika.
"Niwaombe wananchi wa Kigamboni mabadiliko huwa yanakuja na changamoto zake ,leo mnatumia maji ya chumvi ambayo ni yakisima mnaonani ya bei rahisi nikuambieni nisuala la mudatu gharama ya kutumia maji ya DAWASA ni rahisi kuliko hayo ya chumvi ambayo ninyi mnajua mabomba yanaoza sababu ya kutu "Alisema
Aidha ameiagiza DAWASA Kigamboni kuwaunganishia huduma ya maji wananchi wahali yachini kwa mkopo wawe wanalipa taratibu wanapo lipia ankara huku akiwataka kuboresha miundombinu ya mabomba ambayo yemelalamikiwa na wananchi kuwa yanakutu yanatoa kutu jambo ambalo linasababisha maji kuonekana machafu.
Akijibu hoja zilizo tolewa nawananchi amewaagiza DAWASA kutumia lugha nzuri kwa wateja wao na kushughulikia dharu za kukatika, mabomba kupasuka na kutoa taarifa kwa wateja kama inavofanya TANESCO.
"DAWASA acheni kukatia watu maji badala yake shughulikieni matatizo bomba linakatika ukarabati haufanyiki mnakuja kufunga na mpira ,kama mnafunga na mpira sawa fungeni kama huduma ya kwanza lakini siyo mkifunga hivyo ndo mnakaa wiki ,mwezi bila kushughulikia tatizo "Alisema
Hata hivyo Mkuu huyo amewaahidi wananchi kuwa ataitisha mkutano utakao husisha malaka ya uthibi wa maji na mafuta EWURA ili kuweza kujadili suala la bei ambapo wananchi wanalalamikia kuwa bei ya units za maji ni kubwa .
Kwa upande wake Meneja wa DAWASA Kigamboni Tumaini Muhondwa ,akifafanua maswali ya wananchi yaliyo ulizwa mkutanoni hapo amesema suala la kubadilishwa accoumt ya malipo kila mwezi ni utaratibu wa sasa wa Serikali hivyo wananchi waamini kuwa fedha za serikali ziko salama.
Katika kuboresha huduma DAWASA inajenga tank eneo la kisaraweii ambalo kwa sasa limefikia asilimia 30 ya utekelezaji ,na mradi mwingine utaanza kujengwa mwezi februari tank lenye ujazo wa lita milioni 2.

Post a Comment