Ads

TANCDA: Ulaji wa Vyakula halisi husaidia upatikanaji sawa wa Sukari Mwilini

 

Wapili kutoka kulia ni Meneja Mradi wa Shirikisho la Magonjwa Yasiyo ya Kuambukiza (TANCDA) Happy Nchimbi akiwa na maafisa wengine kwenye banda juzi siku ya  ufunguzi wa Kongamano la pili la Kisayansi la maadhimisho ya wiki ya kuzuia na kudhibiti magonjwa yasiyoyakuambukiza Dar es Salaam.

..............................
Maana ya Magonjwa Yasiyoambukiza ni yale yasiyo  na vimelea vinavyoweza  kusambazwa.

 Vipeperushi na vijitabu kutoka TANCDA vinaeleza mfano wa magonjwa hayo kuwa saratani, magonjwa sugu ya njia ya hewa  ,kisukari, magonjwa ya akili na mengine ya kurithi ugonjwa wa selimundu.

 

Kupunguza Magonjwa yasiyo ambukiza inaelezwa kila Mlo uwe na makundi yote matano ya vyakula ambayo ni (a)Nafaka ,Mizizi,Ndizi Mbichi za Kupika (b)Jamii ya Mikunde na Asili ya Wanyama (e)Mafuta.

 

Pia Ulaji wa vyakula halisi husaidia upatikanaji sawa wa sukari mwilini, kwa kuhifadhi na kumeng'enya pole pole chakula tumboni.

 


Jamii pia imeshauriwa kuwa sukari ikizidi mwilini huharibu mishipa ya damu nafahamu, macho ,figo na kongisho hivyo inashauriwa  kutoongeza sukari kwenye vyakula au vinywaji kwani sukari hiyo inapatikana mwilini haraka zaidi ya inavyotakiwa.

 

TANCDA imekuwa ikielekeza pia kupitia vijarida vyake na pamoja na wataalam wake kuwa jumla ya sukari yote ( kwenye vyakula, vinywaji, chai) isizidi vijiko vidogo vya chaivitano kwa mtu mmoja kwa siku.

 

Imeelekezwa kuwa kukamua matunda ili kutengeneza juisi :matunda hukaa tumboni muda mrefu zaidi na kupunguza kasi ya upatikanaji wa sukari mwilini.

 

Kuhusu agizo la Mwenyezi Mungu , Mtakula kwa jasho lenu! Jihudishe na chochote kitakachokufanya utoke jasho angalau kwa nusu saa kila siku.

 

Bila mazoezi ,misuli hupoteza uwezo wa kutumia sukari, husinyaa na mifupa huwa laini na kuvunjika kwa urahisi,mazoezi pia kupunguza msongo wa mawazo na chumvi na mafuta yaliyozidi mwilini.

 

Taamaa mbaya aisee na ukiiga tembo kunya utapasuka msamba ,kuwa na malengo sahihi juu ya maisha yako hapa duniani na fanya yaliyokwenye uwezo na vipaji vyako ilikupunguza msongo wa mawazo na kuepuka kisukari, msukumo wa juu wa damu.

 

Magonjwa yasiyoyakumbukiza yamelisababishia Taifa hasara kubwa kwa kuondoa nguvu kazi na kurudisha nyuma maendeleo ya mtu binafsi na Taifa kwa ujumla.

 

Hayo yameelezwa juzi Jijini Dar es Salaam na Mganga Mkuu wa Serikali Prof. Abel Makubi kwa niaba ya Katibu Mkuu Wizara ya Afya katika ufunguzi wa Kongamano la pili la Kisayansi la maadhimisho ya wiki ya kuzuia na kudhibiti magonjwa yasiyoyakuambukiza.

 

Akizungumza katika Kongamano hilo Prof. Makubi amesema asilimia 33 ya vifo vyote nchini kwa mwaka 2017 vimetokana na magonjwa yasiyoyakuambukiza ikiwemo magonjwa ya moyo na shinikizo la Damu kwa asilimia 13, Kisukari asilimia 2, saratani asilimia 7 na ajali asilimia 11.

 

Aidha amesema hali hiyo haikubaliki hivyo wanapanga mikakati ya pamoja ili kukabiliana na changamoto hiyo ambayo inaongeza utegemezi sugu kwa familia na kuongeza mzigo mkubwa kwenye mfumo wa afya kwa kuwa ni magonjwa ya muda mrefu na yanatumia rasilimali nyingi.

 

Hata hivyo amesema kupitia Kongamano hilo serikali inatarajia kupata mapendekezo ya wadau wa Afya ili kuweza kuimarisha huduma za kuzuia na kudhibiti magonjwa yasiyoyakuambukiza hivyo ni vyema yawe mapendekezo ya kutekelezeka.

 

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Huduma za Tiba Wizara ya Afya Dkt.Grace Magembe amesema kwa takribani miaka nane magonjwa yasiyoyakuambukiza yamekuwa yakiongezeka ikiwa ni pamoja na gharama za matibabu.

 

Aidha ameongeza kuwa lengo la Kongamano hilo ni kutoa uelewa kwa jamii kuhusu magonjwa hayo na njia za kukabiliana nayo ambapo katika wiki ya maadhimisho watatoa elimu kupitia sehemu mbalimbali ikiwemo vyombo vya habari pamoja na kutoa huduma ya upimaji katika viwanja vya Mnazi Mmoja Jijini Dar es Salaam.

 

Takwimu za Shirika la Afya Duniani (WHO) zinaonyesha kuwa magonjwa yasiyoyakuambukiza yanachangia zaidi ya vifo milioni 41 ambayo ni sawa na asilimia 71 ya vifo vyote milioni 57 vilivyotokea mwaka 2016 huku mataifa ya Uchumi wa kati na chini kama Tanzania yakionekana kuathirika zaidi.

 

Meneja Mradi wa Shirikisho la Magonjwa Yasiyo ya Kuambukiza (TANCDA) Happy Nchimbi, amesema wamekuwa wakitoa upimaji wa afya kwa mafanikio.

Anasema Mfano mwaka 2018 walifanya kambi sehemu ya mikoa mbali mbali juu ya upimaji wa afya iliyofanyika katika nyakati za miezi Oktoba 21 na kumalizika Oktoba 28 mwaka huo. 

 

Happy amesema kuwa katika kambi hiyo waliweza kutoa huduma ya upimaji bure wa magonjwa yasiyoambukiza ambao ulifanywa na wao TANCDA na kuwa uliweza kuwapima wananchi zaidi ya 1500 ambapo wanachi waliendelea kujitokeza kupata huduma hiyo.

 

"Wananchi waliweza kufurahi sana  huduma hiyo ambapo wengi wao walikuwa na tatizo la shinikizo la damu bila wao wenyewe kujifahamu, lakini pia wengi waliweza kugundulika kuwa na uzito wa juu,"amesema Happy. 

 

Happy amesema kuwa  wananchi  wanahitaji sana elimu ya magonjwa yasiyo ya kuambukiza na visababishi vyake hasa ulaji usiofaa,ufanyaji mazoezi na kupunguza matumizi ya pombe kwa wingi. 

 

Amesema kuwa katika zoezi hilo Waziri wa nchi ofisi ya TAMISEMI ndiye alikuwa mgeni  rasmi katika moja ya mkoa na alijionea zoezi hilo likiendelea, na kuona uhitaji wake kwa wananchi.

 

Imeelezwa kuwa watu 9 kwa kila 100 ya Watanzania wenye umri wa miaka 25 na  kuendele wana ugonjwa wa kisukari,hata hivyo inatajwa kuwa kati ya hao 9 ni wawili tu wanaojijua kuwa wanakisukari.

 

Hayo yalikuwa ni maneno yake Profesa Swai  mara alipokuwa akifanya mahojiano na mwandishi wa makala hii mwaka 2018  ambapo alipambanua mambo mengi juu ya magonjwa yasiyo ya kuambukiza.

 

Alipambanua kuwa ilikugundua kama unashinikizo kubwa la damu ni vyema kupima msukumo wa damu kila unapoenda kwenye kituo cha tiba au kupima angalau mara moja kwa mwaka.

 

"Kwa mda mrefu tulikuwa tukielimisha ulaji unaofaa kila tunapopata fursa ya kuzungumza na watanzania lakini bado jamii haizingatii ulaji bora na salama," Pia  akakumbusha umuhimu waulaji unaozingatia kiasi na si bora ulaji.

 

Profesa Swai  hivyo aliwataka watanzania kufanya mazoezi kila siku walau dk 30 za kuuweka mwili vizuri ili kukabiliana na magonjwa yasiyo ya kuambukizwa.

 

Kwakuwa magonjwa hayo ndiyo magonjwa yanayoongoza kwa vifo vingi barani Afrika.

Sababu  zinazosababisha ama kuchangia mtu kupata shinikizo kubwa la damu zimetajwa kuwa ni matumizi ya chumvi kupita kiasi hasa ya kuongeza mezani,utumiaji wa pombe kupitakiasi pamoja na utumiaji wa tumbaku na bidhaa zake pamoja na msongo wa mawazo.

 

 Moja ya visababishi vingine inatajwa kuwa ni kutojishughulisha mwili ugonjwa wa kisukari ni moja ya kisababishi katika shinikizo la damu.

No comments