Ads

KIGAMBONI MANISPAA YATOA TENA MIKOPO YA MAMILIONI KWA WAJASILIAMALI

 

Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Sara Msafiri wapili upande wa kulia ,kwanza upande wa kulia ni afisa Maendeleo Manispaa ya Kigamboni  Happy Luteganya wengine 

Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Sara Msafiri wapili kutoka  upande wa kushoto  akikabidhi pikipiki kwa  kikundi Cha Vijana waliokopeshwa Pikipiki na Manispaa ya Kigamboni.

Halmashauri ya Manispaa ya Kigamboni imesema katika kuwainua wajasilia mali wa kigamboni imeanda eneo maalumu ambalo watapewa wajasiliamali kwaajili ya kufanya biashara ambalo pia linatarajiwa kujengwa stand kubwa ya daladala .

Hayo yamebainishwa na mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Sara Msafiri wakati akigawahundi kwa vikundi vya wajasiliamali akinamama ,Vijana na Walemavu ambapo Manispaa hiyo leo imetoa jumla ya shilingi milioni 165,385,000.00 kwa vikundi 26.

Aidha DC  Msafiri amewataka wanufaika wa mikopo hiyo kuzingatia  kurejesha mikopo hiyo ili na wengine waweze kunufaika na mikopo hiyo.

Amesema Serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Magufuli imedhamiria kuwainua kiuchumi wananchi wake ili kuendana uchumi wa kati.

Manispaa ya Kigamboni tangu imetengwa kuwa Wilaya imekwisha toa toa mikopo yenye thamani ya shilingili Bilioni 1,697,600.00 kwa vikundi 486 vyenye jumla ya wanufaika 4680,ambapo jumla ya shilingi 493,092,140.00 zimerejeshwa.


No comments