FEI TOTO AIBEBA TAIFA STARS DHIDI YA TUNISIA YATOKA SARE 1-1 KUFUZU AFCON MWAKANI
Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) imejiweka katika nafasi mbaya ya kufuzu Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) baada ya kulazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 na Tunisia katika mchezo wa Kundi J uliochezwa Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.
Kwa matokeo hayo, Tunisia wanafikisha pointi 10 na kuendelea kuongoza kundi hilo, sasa wakiwazidi pointi nne Equatorial Guinea wanaofuatia, wakati Tanzania inafikisha pointi nne na kusogea nafasi ya tatu ikiiteremshia mkiani Libya yenye pointi tatu baada ya timu zote kucheza mechi nne.
Hadi mapumziko, Carthage Eagles walikuwa mbele kwa 1-0, bao lililofungwa na kiungo wa Olympique de Marseille ya Ufaransa, Saif-Eddine Khaoui dakika ya 11 akitumia makosa ya safu ya ulinzi ya Taifa Stars.
Tunisia waliendelea kutawala mchezo na kucheza kwa utulivu pamoja na kuwaruhusu Taifa Stars kupata bao ka kusawazisha, lakini sifa zimuendee kipa Aishi Manula aliyeokoa michomo kadhaa.
Taifa Stars nayo ilitengeneza nafasi nzuri zaidi ya tatu za kufunga mabao lakini wakapoteza kupitia kwa Iddi Suleiman ‘Nado’, Adam Omary na Ditram Nchimbi.
Kikosi cha Tanzania kilikuwa; Aishi Manula, Shomari Kapombe, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’, Erasto Nyoni, Bakari Mwamnyeto, Jonas Mkude, Himid Mao/Feisal Salum dk35, Ditram Nchimbi, John Bocco, Simon Msuva/Said Ndemla dk80 na Farid Mussa/Iddi Suleiman ‘Nado’ dk80.
Tunisia; Farouk Ben Mustapha, Wajdi Kechrida/Mohamed Drager dk79, Yassine Meriah, Dylan Bronn, Youssef Msakni/ Nabil Makni dk90, Saif-Eddine Khaoui/Naim Sliti dk69, Wahbi Khazri/Hamza Rafia dk77, Ali Maaloul, Ferjani Sassi, Mohamed Ben Amor/Anis Ben Slimane dk90 na Ellyes Skhiri.
Post a Comment