Ads

KUMBILAMOTO AUWASHAMOTO VINGUNGUTI ,BAADA YA KUNUNUA GARI LA WAGONJWA ATOA AHADI NYINGINE


Mjumbe wa baraza kuu Taifa UVCCM Gwantwa Alex , akimnadi mgombea wa kiti cha udiwani kata ya Vingunguti Omary Kumbilamoto aliyevaa kofia ya kijani

Mjumbe wa Barazakuu Taifa UVCCM Gwantwa alex, akizungumza katika mkutano wa kampeni  kata ya Vingunguti ambapo alimwombea kura  wagombea wa CCM  Omary Kumbilamoto kuwa diwani ,Mgombea ubunge jimbo la Segerea Bonna Kamori  na Mgombea urais  CCM Dkt John Pombe Magufuli.

Mgombea udiwani kata ya Vingunguti Omary Kumbilamoto,  akiomba kura katika mkutano wa kampeni uliofanyika mtaa wa Mwembeni Vingunguti (Picha zote na Mwamba wa habari)




Mjumbe wa Barazakuu Taifa UVCCM Gwantwa alex, akizungumza katika mkutano wa kampeni  kata ya Vingunguti ambapo alimwombea kura  wagombea wa CCM  Omary Kumbilamoto kuwa diwani ,Mgombea ubunge jimbo la Segerea Bonna Kamori  na Mgombea urais  CCM Dkt John Pombe Magufuli.

Aliyekuwa Meya wa Manispaa ya Ilala ambaye pia ni mgombea  udiwani kata ya Vingunguti amewataka wananchi wa kata hiyo kuwachagua wagombea wa CCM kwani wako mstari wa mbele katika kuleta maendeleo na kuongeza kuwa mnamo siku ya Jumatatu   ujenzi wa Barabara ya Vingunguti Barakuda  unatarajiwa kuanza rasmi  . 

 Kumbilamoto ameyasema hayo wakati wa mkutano wa Kampeni za udiwani wa kata hiyo ambapo alikuwa akiomba kura za chama cha Mapinduzi za Rais John Magufuli na Mbunge Bonah Ladslaus Kamoli.

"Kero ya barabara ya Vingunguti kuanzia Scania mpaka TABATA Barakuda imepata ufumbuzi ujenzi wake unaanza mara moja kuondoa kero ya barabara hii Mh, Rais John Magufuli ameshatoa shilingi bilioni 2 za matengezo na kama fedha aijatosha atatoa pesa nyingine kuakikisha WANANCHI Vingunguti wanatumia barabara nzuri yenye kiwango "alisema Kumbilamoto. 

Kumbilamoto aliwaomba October 28/2020 kura zote CCM kwa John Magufuli na Mbunge Bonah Ladslaus Kamoli msifanye kosa tuchague viongozi hawa tuletewe maendeleo kwa kasi katika kujenga TANZANIA ya Uchumi wa viwanda. 

Alisema serikali imetenga bilioni 140 kwa ajili ya miundombinu Wilaya Ilala, na Bilioni 32 kwa ajili ya bonde la Msimbazi kwa ajili ya kuweka kingo mto Msimbazi.

Aliwataka wamchague kwa ajili ya Maendeleo Ilala na Vingunguti ambapo mara atakapochaguliwa atasimamia ujenzi wa mradi wa barabara za kisasa DMDP katika kata hiyo. 

Aidha alisema katika kipindi chake cha miaka mitano  ameweza kusimamia mradi wa serikali wa Machinjio ya Vingunguti ambapo kwa sasa upo katika hatua za mwisho mradi uliogharimu shilingi bilioni 12  ,pia amesimamia sekta ya elimu kwa kuboresha elimu na mazingira ya shule na ujenzi wa sekondari. 

Pia alisema mengine ambayo amefanya ni kuboresha setka ya afya ikiwemo kununua gari la wagonjwa Zahanati ya Vingunguti na kuboresha Ofisi za Chama cha Mapinduzi CCM ndani ya Kata hiyo. 



No comments