Viongozi wa Vyama vya Siasa waaswa kufanya kampeni za kistaarabu kudumisha amani Uchaguzi Mkuu 2020.
Viongozi wa Vyama vya Siasa nchini wameaswa kufanya kampeni za kistaarabu katika kipindi hiki cha Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Oktoba 28 mwaka huu ili kuendelea kudumisha amani na utulivu.
Kauli hiyo imetolewa jijini Dar es Salaam Dar es Salaam na Sheikh Hemed Jalala katika Matembezi Amani ya Link in buna Mjukuu wa Mtume (Imam Hussein).
Alisema matembezi hayo yanafanywa kumkumbuka Imam Hussein aliyekufa miaka 1400 iliyopita na kwamba kiongozi huyo alihimiza umoja ,mshikamano bila kujali itikadi za kidini na rangi hivyo kampeni uchaguzi zifanyike kwa amani.
"Hussein alitunza umoja ,mshikamano bila kuangaliaitikadi za dini wala vurugu kampeni zifanyike kwa kujali mustakabali wa amani yetu ," alisema Sheikh Jalala.
Sheikh Jalala alifafanua kuwa kiongozi wanatakiwa kuzungumza lugha safi zisizoleta chuki badala yake wahimize lugha za kistaarabu zitakazosaidia kujenga umoja na mshikamano.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Jumuiya za Khoja Shia Azim Dewji alisema siku ya Ashura inaombolezwa duniani kote kumkumbuka Imam Hussein kwa msimamo wake wa kusimamia haki.
Aliishukuru Serikali kwa kuipa jumuiya hiyo kibali cha kufanya matembezi hayo kila mwaka na kwamba inaonesha jinsi inavyothamini mchango madhehebu ya katika kudumisha umoja na amani.
Naye Sheikh kutoka Jumuiya ya Mabohora Daudi Khatibu alisema matembezi hayo yanahamasisha jamii kumuenzi Imam Hussein kwa kudumisha umoja na mshikamano pamoja na kupinga ubaguzi na dhuluma.
Sheikh Khatibu alisema anaamini uchaguzi utafanyika kwa amani bila kuvuruga umoja na mshikamano ulliopo nchini.
Post a Comment