Mgombea Ubunge CCM Kigamboni Dkt Faustine Ndugulile atoa matumaini makubwa kwa wanakigamboni
Na John Luhende
Mwamba wa habari
Mgombea kiti cha ubunge jimbo la kigamboni Dkt Faustine Ndugulile akiwa katika mkutano wa kampeni na makamu wa Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan amesema, ndani ya miaka mitano Kigamboni imefanikiwa kuvusha Bomba kutoka Ruvu chini sasa wananchi wa Kata ya Tungi na maeneo jirani wanapata majisafi na salama .
"Mradi wa visima unaofahamika Kama kimbiji ulioko kisarawe ll unagharimu jumla ya shingi billion 12.4 utakuwa na uwezo wa kutoa Lita million 44 kwa siku na mahitaji Lita 24" Amesema
Wakati Serikali hii inaingia madarakani Umeme ulikuwa unakatika Katika Sasa kuna moja ya umemem sasa kuna line mbili zimeunganishwa kutoka mbagala na kurasini unagharimu jumla ya shilingi billion 26 mradi huu unakamilika mwezi oktoba mwaka huu,
Kigamboni ina Mitaa 67 , mitaa 31 imepatiwa umeme mitaa Iliyobakia nayo itapatiwa umeme karibuni .
Wilaya ya Kigamboni Ilianzishwa mwaka 2016 kielimu ilikuwa chini Sana Sasa Kigamboni kielimu shule ya msingi iko katika kumi Bora , pia tumejenga shule mpya za 3Alevel yaani kidato cha tano na sita.
Miundo mbinu ya barabara tuna kilomita 883 kiwango cha changarawe kilomita 1.8 lami na kilomita 142 ziko chini ya Tanroads .
Katika Maendeleo Mradi wa mji mpya ulichelewesha Maendeleo ,tunamshukuru Rais Magufuli kwa kuivunja KDA, wananchi mkiichagua CCM tutajenga barabara na tatu na ku sambaza maji ya DAWASA ikiwemo kuunganisha umeme kata na mitaa yote .
Tunataka kitovu Cha viwanda kiwe Kigamboni na tunamaeneo ya kutosha , tumetumia milioni 75 kujenga soko la samaki Pemba mnazi ili kuendeleza shuguli za uvuvi.
"Wavuvi wa Kigamboni wamezuiwa kuvua mchana nakuomba Makamu ulichukue Ila siyo kwamba tunaunga mkono uvuvi haramu"
Kigamboni Ina kata 9 na tuna Ambulance 3,vivuko , darajani nalo limekamilika na barabara zingine zinaendelea kujengwa .
Miundo mbinu ya barabara tuna kilomita 883 kiwango cha changarawe kilomita 1.8 lami na kilomita 142 ziko chini ya Tanroads.
Mwisho Dkt Ndugulile amewataka wanankigamboni kumchagua kuwa mbunge na kumpa kura za urais Dkt Magufuli na kuwachagua madiwani wa CCM .
Post a Comment