Ads

Maneno ya Mgombea mwenza CCM, Mama Samia Suluhu akiomba kura Kigamboni

Mgombea mwenza Urais CCM Samia Suluhu Hassan akizungumza katika mkutano wa kampeni wilaya ya kigamboni ,aliyeko kulia ni Mgombea Ubunge jimbo la Kigamboni Dkt Faustine Ndugulile akionesha Ilani ya uchaguzi ya CCM baada kukabidhiwa (Picha na Mwamba wa habari)

Na John Luhende

 Nilianza ziara ya kuomba kura Dar es salaam tarehe 5  kwa  Wilaya  za Ilala na Temeke, leo niko Kigamboni  na nitarudi tena Ubungo na Kinondoni ,kote nilikopita nimejionea Maendeleo ya miradi ilitotekelezwa na serikali  ya awamu ya tano.

Wakati napitia ilani ya uchaguzi,  nimeona yote tumetekeleza  ,mbunge kasema yote yaliyo tendeka Kigamboni, sikutaka nieleze mimi nimemwachia Mbunge nyie wenyewe mmemsikia .

  Dar es salaam tumetumia bilioni 40 kwaajili ya elimu  bure , ujenzi , ukarabati wa shule ,vyuo vikuu  tumetoa mikopo mkiichagua tena  tutaendelea na Kasi ile ile tunampango wa kujenga vyuo 2 vya walimu  hapa Dar es ili tuweze kuzalisha walimu zaidi .

MEMKWA  ili watoto wetu waweze kusoma na kipata elimu bora , tutaendelea kujenga madaraja na bara bara mfano Sasa tunajenga barabara nane  Ubungo  Dar es Salam nimji wa kibiashara  lazima uwe na miundo mbinu mizuri.

Daraja la Nyerere limeshakamilika  na lile la Salenda tutaendelea kulijenga ,huduma ya  Hospital na vituo vya afya ,umeme na Maji tutaendelea kuimarisha , DAWASA tutawakabidhi kazi na wanafedha zote ili kutekeleza miradi ya Maji .

Usafiri wa Anga ,bara bara na bara bara  za juu tunaendela kujengwa na makutano zote mfano  ,uhasibu ,mwenge Chang'ombe  na maeneo mengine pamoja ujenzi   barabara zingine ,kawe , Morocco ,Ardhi chuo kikuu huko Makongo.

Kigamboni bara bara nyingi zinazo hudumiwa na TARURA nimbovu ,Wilaya za Ubungo na Kigamboni zita kuwa na Mradi wa DMDP ili kuimarisha  huduma  pia jangwani kutajengwa kisasa  ili kuzuia mafuriko,na pia kunamradi wa mwendo Kasi mbagala Morocco na mwenge .

Ujenzi wa Reli tunakamirisha kipande Cha Dar - Moro,  Sasa kimefikia   asilimia 75, na pia  tunatarajia  kuanza kwa ujenzi wa kipande kutoka Dodoma mwanza  .

Anga, ndege zimenunuliwa tunajipanga kuongeza ndege zaidi zikiwemo za mizigo.

Nishati tutaendelea na miradi ya umeme vijini  REA ,kumalizia ujenzi wa Bwawa la Nyerere ili kuimarisha huduma  za umeme ,na tutatimiza ahadi yetu  ya kituo Cha afya Kila kata .

Viwanda ,Sera ya viwanda tunaendela nayo na Kila mkoa umetenga maeneo ya viwanda  ili kukuza uchumi na kuongeza ajira kwa kwa watu wetu .

Uvuvi Katika ukanda wa Pwani, kunauwezekano mkubwa tutajenga kiwanda kikubwa Dar es salaam,nimeambiwa kunachangamoto ya wavuvi kuvua mchana niachieni hili ntalifanyia kazi litakwisha .

Tunajipanga kununua Meli tano za uvuvi ili ziweze kuvua tukuze kipato ,tutaweka mazingira Bora kwa wavuvi wetu.

Utalii ,tumejipanga kuipa hadhi Tanzania kwa kuutangaza  utalii  tunatarajia kupokea watalii wengi zaidi kufikia milioni 5,Katika miaka mitano, tunategemea kutekeleza hayo na yote yaliyopo Katika Ilani yetu yote yapo ndani ya uwezo wetu tunamuomba Mungu atusikie atuwezeshe .

No comments