TRA KUJENGA MAZINGIRA RAFIKI KWA WAFANYABIASHA.
Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA)imesema itahakikisha inajenga mazingira rafiki kwa wafanyabiashara ikiwemo kufanya mazungumzo nao ili kuwasaidia kulipa kodi kwa wakati na Nchi kujiongezea Mapato.
Akizungumza na Waandishi wa Habari Jijini Dar es salaam Mkurugenzi wa Elimu kwa Mlipa Kodi (TRA) RICHARD KAYOMBO amesema Mamlaka hiyo septemba mwaka huu inaendelea na kampeni ya Elimu kwa wafanyabiashara katika Mikoa ya Arusha,Mtwara,Dar es salaam,Kagera Tabora lengo ni kufanya mazungumzo nao kubaini changamoto zinazowakabili na kuwapatia mwongozo wajisajili na kuwaondoa hofu.
Sanjari na hayo amesema kampeni hiyo ya robo ya mwaka hupita kwa kila mfanyabiashara mmojamoja na kuwapatia Elimu namna na kuepuka kutoingia katika mtego wa kukiuka kanuni na taratibu zinazopelekea kulipishwa faini baada ya kuchelewa kulipa kodi kwa wakati
Hata hivyo alisema TRA imeanzisha mfumo wa kumrahisishia mfanyabiashara kuweka taarifa zao Mtandao kwa kujisajili na kulipa kodi popote walipo hali hiyo inasaidia kuondoa usumbufu wa kufika mamlaka na kuondokana na matapeli waliokuwa wanatumia jina la TRA na vitambulisho feki kutapeli watu.
Aidha TRA inawakumbusha wale wote umetolewa kwa waajiriwa na kuhakikisha wanajisajili kuwa na tin namba na zoezi Hilo dirisha la kujisajili litaendelea Hadi desemba 31 mwaka huu na ambaye atakutwa Hana tini namba sheria kali itachukuliwa dhidi yao .
Post a Comment