Ads

Chuo Kikuu Huria Nchini chawakaribisha wanafunzi wenye sifa kujiunga na mwaka wa masosmo 2020/21

Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (OUT) kimesema kinawakaribisha wahitimu wenye sifa wa kidato cha sita, na Astashahada kujiunga na chuo hicho katika programu mbalimbali kwani watatoa elimu bora kutokana na mifumo thabiti ya usomaji na ufundishaji ikiwemo ya njia ya mitandao.

Chou hicho kimewakaribisha wanafunzi kujiunga na kozi mbalimbali, ambapo wanafunzi watakaojiunga watapata faida ya kusoma na kujifunza kwa vitendo kwa kutumia miundo mbinu bora.

Hayo yalisemwa Dar es Salaam jana na Mkurugenzi wa Mahusiano Masoko wa  chuo hicho Dkt. Mohamed  Maguo kwenye maonesho ya Elimu ya Juu, Sayansi na Teknolojia yanayofikia kilele kesho kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja .
Mkurugenzi wa Mahusiano na Masomo wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania akizungumza na wanafunzi juu ya kuwakaribisha wahitimu kidato cha sita kujiunga na program za masomo katika Maonesho ya Elimu ya Juu, Sayansi na Teknolojia yanayofikia kilele kesho Viwanja vya Mnazi, jijini Dar es Salaam.

Alisema watakaojiunga na programu mbalimbali katika chuo hicho watapata faida katika kusoma kwa kujifunza kwa vitendo kwa kutumia miundo mbinu bora ikiwemo kupitia tehama .

"Kuna matawi ya OUT kwa kila mkoa ambapo mwanafunzi hana haja ya kuja makao makuu anasoma na kujifunza huko alipo tunawalimu waliobobea na mifumo bora ya ufundishaji  hasa hasa ya mitandaoni ," alisema Dkt.Maguo.


Alisema OUT kinawakaribisha wanafunzi wa kidato cha sita na ngazi zingine waliopungukiwa sifa ya kujiunga na shahada ya kwanza kwani  waliokosa sifa wataweza kupata kozi inayowawezesha kujiunga, hivyo watasoma mwaka mmoja ndipo watajiunga na shahada hiyo katika chuo chochote kilicho nchini au nje ya nchi.

Dkt. Maguo alisisitiza kwa wahitimu wa kidato cha nne wasio na sifa wanapewa nafasi kujiunga na OUT kwa kupitia kozi hiyo na watapomaliza watakuwa na uwezo kusoma ngazi ya cheti katika chuo chochote au nje.

Alifafanua kuwa mhitimu wa kidato cha sita aliyepata daraja la tatu la pointi 14 atalazimika kusoma kozi hiyo (Foundation Course) kwa mwaka mmoja, ndipo  kuendelea na masomo ya shahada ya kwanza huku wale waliomaliza Astashahada waliopata chini ufaulu wa G.P.A ya 3.0 watasoma kozi hiyo.

Pia kozi hiyo ni pamoja na waliomaliza ngazi ya cheti NTA level 5 waliosoma miaka mitatu wataingizwa kwenye kozi hiyo .

Alisema kuwa chuo hicho kilianzishwa mwaka 1992 kwa sheria Na17 ya Bunge inayokipa maelekezo ya kutoa elimu ya juu kwa njia huria na masafa na kusisitiza bado kuna nafasi nyingi za kujiunga pasipo gharama yoyote ya maombi.

Aliongeza kuwa wahitimu wa kidato cha sita,Astashahada, cheti waliokosa sifa ya kujiunga shahada ya kwanza watalipia ada ya Sh 720,000 kwa kozi ya mwaka mmoja itakayomwezesha kujiunga shahada ya kwanza (Foundation Course) huku waliomaliza ngazi ya cheti watalipa sh milioni 2.4.

Dkt.Maguo alisema kwa mwaka wa masomo 2020/21 wanategemea kudahili wanafunzi 16,000 mpaka 20,000 na kwamba chuo hicho kina wanafunzi 60,000 huku wanaosoma ana kwa ana wahitimu ni 20,000 na 40,000 ni wale wanaoahirisha mwaka wa masomo.

Katika hatua nyingine ,Dkt.Maguo alisema OUT kina program zaidi ya 100 kuanzia ngazi ya cheti hadi shahada ya Uzamivu pamoja na kozi takribani 1,000.

Pia alisema wanafunzi watakaosoma OUT watapata fursa ya kujisomea kupitia maktaba ya mtandao kwa ruhusa kuingia pale anapolipia ada ,ratiba ya mafuzo ya ana kwa ana kwa wanafunzi wenye vikwazo watakutana na walimu wao popote walipo.

Vile vile, alisema wanafunzi wa chuo hicho wameunda makundi ya mtandaoni ya majadiliano ya programu mbalimbali (Whatsapp discussion) ambapo kuna viongozi ndani yake hujadiliana masomo na pale panatokea changamoto huwasiliana na walimu wao kuzitatua.

Dkt. Maguo alisema makundi hayo yatawaunganisha wanafunzi wanaosoma OUT kujifunza mtandaoni na limepewa jina la WhatsApp ni kimbweta kwa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania.

5 comments:

  1. CHUO KIZURI SANA MUNGU AWABARIKI SANA.

    ReplyDelete
  2. Nina cheti cha veta vc2 naweza kuja kusoma diploma?

    ReplyDelete
  3. Nakuja kusoma foundation course

    ReplyDelete
  4. Ada inalipwa kwa awamu ngap

    ReplyDelete
  5. Nimesema diploma In primary education, ODPED NAWEZA KUDAHILIWA kusoma digree ya kwanza?

    ReplyDelete