Ads

TFF YAMFUNGIA LUC EYMAEL.

                           .....................
Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kupitia Kamati ya maadili  leo imetangaza kumuadhibu aliyekuwa kocha mkuu wa Yanga SC raia wa Ubelgiji Luc Eymael kwa kumfungia miaka miwili kufanya kazi za soka nchini.

Pamoja na adhabu hiyo aliyopewa Luc Eymael amepigwa faini ya Tsh milioni 8 kutokana na makosa yake aliyoyafanya Kwa kutoa kauli zilizotafsiriwa kuwa za kibaguzi wa rangi.

No comments