Ads

RAIS MHE. DKT.JOHN POMBE MAGUFULI APOKEA HATI ZA UTAMBULISHO KUTOKA KWA BALOZI WA MAREKANI HAPA NCHINI PAMOJA NA VIET NAM, IKULU JIJINI DAR ES SALAAM.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika mazungumzo na Balozi wa Marekani hapa nchini Donald John Wright mara baada ya kuwasilisha Hati za Utambulisho kwake katika hafla fupi iliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimsikiliza Balozi wa Marekani hapa nchini Donald John Wright mara baada ya kuwasilisha Hati za Utambulisho kwake katika hafla fupi iliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam.

Balozi wa Marekani hapa nchini Donald John Wright akiwa amesimama wakati nyimbo za Mataifa mawili ya Tanzania na Marekani zilipokuwa zikipigwa na Brass Band ya Polisi katika mapokezi yake Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Profesa Palamagamba Kabudi katika picha ya pamoja na Balozi wa Marekani hapa nchini Donald John Wright Ikulu jijini Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Profesa Palamagamba Kabudi katika picha ya pamoja na Balozi wa Viet Nam hapa nchini Nguyen Nam Tien mara baada ya kuwasilisha Hati za Utambulisho kwake katika hafla fupi iliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika mazungumzo na Balozi wa Viet Nam hapa nchini Nguyen Nam Tien mara baada ya kuwasilisha Hati za Utambulisho kwake katika hafla fupi iliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam.
PICHA NA IKULU

No comments