Ads

DKT MAGUFULI ACHUKUA FOMU YA KUGOMBEA KITI CHA URAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA LEO JIJINI DODOMA

. 
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa ameshika Begi leye Fomu ya Kugombea nafasi ya Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Tiketi ya CCM katika Uchaguzi Mkuu utakaofanyika tarehe 28 Oktoba, 2020 pamoja na Mgombea Mwenza Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan mara baada ya kuchukua Fomu hizo


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akisaini Kitabu mara baada ya kuchukua Fomu hizo za Kugombea Urais katika Ofisi za Makao Makuu ya NEC Njedengwa leo jijini Dodoma kulia ni Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Dk. Wilson Mahera Charles
 Mgombea wa Urais  Dkt. John Pombe Magufuli na Mgombea
Mwenza katika Uchaguzi Mkuu Mhe Samia Suluhu Hassan wakionesha fomu za
udhamini kwa wanachama wa CCM wa Dodoma baada ya kutoka kuchukua fomu
hizo za kugombea Urais
 Mgombea Mwenza kwa Tiketi ya CCM Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan akisaini kitabu katika Ofisi za Makao Makuu ya NEC Njedengwa leo jijini Dodoma kulia ni Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Dk.Wilson Mahera Charles
Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Mh. Jaji wa Rufaa (Mst), Semistocles Kaijage akizungumza  kabla ya kukabidhi fomu za kugombea kiti cha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Kwa Mgombea wa Chama cha Mapinduzi(CCM) Dk. John Pombe Magufuli (kushoto) katika Ofisi za NEC, 
Njedengwa leo Jijini Dodoma
 Mgombea Urais wa CCM, Rais Dk John Magufuli akizungumza na viongozi, wanachama na wapenzi wa chama hicho katika makao makuu ya chama hicho jijini Dodoma baada ya kutoka kuchukua fomu ya Urais.
 Mgombea Urais wa CCM ambaye pia ni Rais Dk John Magufuli na Mgombea Mwenza ambaye ni Makamu wa Rais, Mama Samia Suluhu Hassan wakimkabidhi Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dodoma,Godwin Mkanwa fomu za udhamini kwa ajili ya kuomba wadhamini wa kuwadhamini mkoani Dodoma.
 Mgombea Urais wa CCM, Dk John Magufuli akionesha kwa wanachama wa chama hiyo fomu ya kugombea Urais ambayo ametoka kuichukua Tume ya Uchaguzi (NEC)leo Jijini Dodoma
Mgombea Mwenza wa Urais wa CCM, Mama Samia Suluhu Hassan akizungumza na wanachama wa chama hicho Makao makuu ya CCM Dodoma.
                                   ...........................................................
Na. Alex Sonna, Dodoma
MwenyeKiti wa Chama cha Mapinduzi(CCM) Dkt. John Pombe Magufuli ambaye pia ni Mpeperusha bendera ya Mgombea Urais  CCM leo  amechukua Fomu za kugombea ili kutetea kiti chake cha Urais.
Akizungumza katika viwanja vya CCM White House,Dkt.Magufuli ameeleza kuwa ameamua kuchukua fomu yeye na Mgombea Mwenza Makamu wa Rais  Samia Suluhu Hassan katika kipindi kingine cha miaka mitano  ili kukamilisha  miradi mingi ya maendeleo waliyoianza kwa awamu yao ya kwanza .
Aidha Dkt. Magufuli ameeleza kuwa wamefanya  mambo mengi katika kipindi hiki,wamejenga shule za msingi Zaidi ya 908,shule za sekondari Zaidi ya 228 ,vituo vya afya Zaidi ya 500,mambo mengine mengi.
“Ukiangalia Dodoma tu ,tumefanya upanuzi wa uwanja wa ndege ,tumweka taa za barabarani,majengo mengi yamejengwa ,kuna program ya kujenga barabara ya njia nne yenye urefu wa kilometa 110 ambayo imetengewa Zaidi ya shilingi bilioni 700,uwanja wa ndege wa Msalato umetengewa shilingi milioni 600,fedha hizi zipo”, amesema Dkt. Magufuli.
“Hivyo  nikiangalia sioni mwingine wa kuja kuyafanya hayo ,tunajenga reli ya mwendokasi ambayo ujenzi wake umefikia asilimia 87 kwa kipande cha kutoka Dar es  Salaam hadi Morogoro na kpande cha Morogoro-Dodoma ujenzi wake umefikia asilimia 32 na tunahitaji tuendelee mpaka Mwanza,nikiacha,yataachiwa pale ,ndio maana nimeona tugombee tena na  Mama Samia.”amesisitiza Dkt. Magufuli.  
Katika hatua nyingine Dkt. Magufuli ameeleza kuwa  katika kipndi chake cha miaka mitano umeme umesambazwa katika vijiji 9,402 kutoka vijiji 3,000 wakati tunaingia madarakani ,vimebaki vijiji 3,000 ambavyo alisema havitamshinda kuvifikia kwa miaka mitano.
Naye Mgombea Mwenza wa Dkt. Magufuli,  Makamu wa Rais Mama Samia amempongeza Rais Magufuli kwa kuhakikisha vifo vya akina mama na Watoto kupungua kutokana na ujenzi wa vituo vya afya nchini lakini pia amepunguza tatizo la upatikanaji wa maji ambapo sasa yanapatikana kwa asilimia 74 na kutoa elimu bila malipo.
Kwa upande wake Katibu Mkuu  CCM Dkt.Bashiru Ally chama hicho kimewasha mitambo yake rasmi huku akitoa majukumu kwa jumuiya za chama hicho.
“Mitambo ya kuhakikisha CCM inashinda imewashwa rasmi leo,muda wa kutesti mitambo umeisha , sasa ni kazi ya kulinda kura,kuhamasisha wapiga kura nyumba kwa nyumba ,kitanda kwa kitanda kwenda kupiga kura,na jukumu hili nalikabidhi kwa UVCCM,
Dkt. Bashiru ameeleza kuwa Mitambo hii ya kisasa inahitaji Mafuta,ikiishiwa maji inahitaji maji ya kupoozea,jukumu hilo amemkabidhi  kwa UWT na mwendeshaji wa mitambo hii ni Jumuiya ya Wazazi.
“Kwa hiyo nakuhakikishia Mwenyekiti safari ushindi utakuwa ni wa kishindo kikubwa ,udiwani tutaongoza Halmashauri zote nchi nzima ,tutakuwa na wabunge wengi kwa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Baraza la Wawakilishi ,na urais Zanzibar tutashinda mchana mapema.”amesisitiza Dkt. Bashiru.




No comments