WARUNDI WAMETAKIWA KUENZI JITIHADA ZA RAIS PIERRE NKURUNZIZA.
Shirika la Elimu ya Amani (EA) imeitaka Serikali ya Burundi kuendelea kuenzi jitihada za Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza kwenye siasa na mageuzi katika nchi na kazi nzuri aliyoifanya enzi ya uhai wake.
Wito huo umetolewa na Mwenyekiti wa Afrika Mashariki, Anthony Mkama Jijin Dar es salaam wakati akifanya mahojiano na mwandishi wa habari amesema Serikali na wananchi wa Burundi inawapasa kuendelea kufuata mienendo mizuri ambayo rais huyo aliyokuwa akiifanya katika kuleta maendeleo nchini humo
"Natoa wito kwa Serikali ya Burundi kuendelea kuenzi mchango na kazi njema aliyoifanya katika jitihada za kuleta maendeleo mazuri ya kisiasa, kiuchumi na kijamii." Amesema.
Hata hivyo Mwenyekiti huyo kwa niaba ya Shirika ametoa salamu za pole kwa Serikali na wananchi wa Burundi kwa msiba uliotokea wa Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza.
"Natoa pole kwa Serikali, wanashirika wa Elimu ya Amani, pia natoa pole kwa wananchi wote wa Burundi kwa kufiwa na Kiongozi wao wa nchi Mungu awatie nguvu katika kipindi hiki kigumu.
Katika hatua nyingine Shirika la Elimu ya Amani Afrika Mashariki, Mwenyekitikama anawapongeza na kuwashukuru wananchi wa Burundi kwa kufanya uchaguzi Mkuu kwa Amani na utulivu.
"Tunashukuru wananchi wa Burundi kwa kufanya uchaguzi Mkuu kwa Amani na utulivu kwa kuzingatia Sheria na taratibu zilizowekwa katika nchi, hii inaonesha moyo wa uzalendo Mungu awabariki Sana." Amesema.
Upande wake Juliana Mushi Katibu Mkuu Afrika Mashariki wa Shirika la Elimu ya Amani amesema wananchi wa Burundi wanatakiwa kuwa na mshikamano na kutoa ushirikiano kwa Viongozi wapya waliochaguliwa ikiwemo Rais, Wabunge, Madiwani na Wenyeviti wa mtaa waliochaguliwa kwenye uchanguzi Mkuu mwezi uliopita.
"Wananchi wa Burundi wawe na umoja na mshikamano pamoja na kuwapa ushirikiano viongozi waliochaguliwa hivi karibuni, suala la kutunza amani lipo mikononi mwao ni jambo jema kutunza na kuilinda amani iliyopo."Amesema.
Post a Comment