KIGAMBONI YAPITISHA AZIMIO KUPONGEZA RAIS KWA MAPAMBANO DHIDI YA COVID 19
Mwamba wa habari
Baraza la Madiwani Manispaa ya Kigamboni kwa kauli moja liemepitisha azimio la Kumpongeza Rais Wa Jamhuri Ya Muungano Wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, Kwa Namna Alivyoliongoza Taifa Katika Mapambano Dhidi Ya Janga la UgonjwaWa Corona (Covid-19)
"Katika kukabiliana na ugonjwa wa Corona Rais alitumia mbinu na mikakati mbalimbali ikiwemo kukataa kuiga mtindo na mbinu ya kufunga mipaka na kuwafungia wananchi wake wasitoke nje tofauti na viongozi wa Mataifa mengine waliofunga mipaka ya nchi zao na kuzuia watu wao kutokanje (Lockdown) "Alisema DC Msafiri.
Aidha alisema kwa kuzingatia hali hiyo, Rais Magufuli aliruhusu shughuli za kiuchumi na baadhi ya shughuli za kijamii ziendelee kwa tahadhari na kuwahimiza wananchi kuzingatia maelekezo na miongozo ya wataalam.
''Waheshimiwa Madiwani sipati picha ikiwa ingewekwa lockdown wananchi wetu hapa kigamboni ingekuwa maana shughuli zao zinategemea hadi wavuke upande wa pili wapate chakula au pata picha Dar es salaam hatulimi magari yote kutoka mikoani yanayoleta chakula yangezuiwa tungekula nini hali ingekuwa mbaya sana"Alisema
Wakitoa michango ya ya mawazo kuhusu mjadala wa azimio hilo baadhi ya Madiwani akiwemo Diwani wa kata ya Tungi aliesema Rais Magufuli amesaidia kuwaondoa hofu Watanzania Diwani wa kata ya Kigamboni Dotto Msawa , alitoa pongezi kwa kuruhusu ibaada huku Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kigamboni Maabadi Suleimani Hoja akisema Rais Magufuli amekuwa Mzalendo wa Kweli kwa Taifa.
Post a Comment